“MATAMSHI ya wandani wa Rais William Ruto kuashiria njama za kuingilia uchaguzi wa 2027 ili kumpendelea kiongozi wa taifa, yameibua upya maswali kuhusu uhuru wa tume ya uchaguzi. Gumzo kuhusu kuiba kura liliendelea wikendi wakati Naibu Gavana wa Kakamega Ayub Savula na mbunge wa Hamisi Charles Gemose, waliwaambia wazi wajumbe wa chama tawala UDA wanaotoka eneo la Magharibi wasaidie katika kuvuruga matokeo ya uchaguzi kwenye vituo vya kupigia kura maeneo yao siku ya uchaguzi Agosti 9. Wanasiasa hao walidai kuwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ni kiungo cha serikali kwa sababu inategemea “bajeti kutoka serikali ya Rais Ruto,” na hivyo haiwezekani kwake kushindwa katika kinyang’anyiro kitakachoendeshwa na taasisi hiyo. “Nataka nyinyi kama wajumbe wa UDA mnapoenda kwenye vituo vya chaguzi (2027), mhakikishe mnamfanyia ukarabati Ruto. Nimekuwa bungeni kwa mihula mitatu na ninajua mambo haya (kuingilia),” alisema Bw Gemose. Bw Savula said: “Ni sisi (serikali) tunalipa IEBC na makamishna. Ruto ndiye anayemiliki bajeti inayofadhili IEBC. Mna kichaa ikiwa mnafikiri anaweza kushindwa kwenye chaguzi. Matamshi hayo yaliyotolewa mbele ya Gavana wa Bungoma Ken Lusaka, anayeongoza kampeni ya Dkt Ruto eneo hilo, yameongeza mdahalo wa umma unaozidi kuchacha kuhusu njama za kuingilia chaguzi za 2027. Lakini akizungumza na Taifa Leo jana, Bw Savula alisema matamshi yake yalitafsiriwa visivyo. Alisema hakuna mpango wa kuiba kura. Si mara ya kwanza wandani wa UDA wanatoa matamshi kama hayo. Mwaka uliopita, Mwakilishi Mwanamke Wajir, Fatuma Abdi Jehow, alisema eneo la Kaskazini Mashariki litahakikisha Rais Ruto anapata muhula wa pili afisini hata ikibidi kuvuruga matokeo. Wabunge Oscar Sudi (Kapsaret), William Kamket (Tiaty), Farah Maalim (Dadaab) na mwenzake wa Baringo Kaskazini Joseph Makilap vilevile wametoa matamshi sawia hapo awali. Vinara wa upinzani jana walitaja matamshi hayo kama ya kiholela yanayoweza kutumbukiza taifa kwenye machafuko kisiasa sawia na kilichoshuhudiwa 2007. Aidha, walitaja wito wa kuingilia chaguzi kuwa ithbati kwamba UDA haiwezi kushinda uchaguzi katika ushindani wa haki. Mwenyekiti wa IEBC Erastus Edung Ethekon hakujibu maswali yetu kuhusu iwapo tume hiyo itawachukulia hatua wanasiasa wanaozungumza kuhusu kuvuruga chaguzi. Kamishna anayeketi kwenye Kamati ya Oparesheni, hata hivyo, alihakikishia Wakenya kwamba wangali huru katika kutekeleza majukumu yao Wanasiasa wa upinzani, hata hivyo, walisema hali kwamba tume haijachukua hatua kali ni ishara kwamba imetekwa. Gavana wa Siaya na kinara mwenza wa Linda Mwananchi, James Orengo, alieleza Taifa Leo kuwa baadhi ya makamishna waliletwa afisini na watu walio serikalini. “Ni sharti wapatiwe ilani kuwa hatutakubali ubaguzi katika uchaguzi huu. Tumezua masuaa, baadhi kuhusu shirika la teknolojia ya uchaguzi Smartmatic. Litakuwa janga ikiwa wanataka kufanya walichofanya katika chaguzi za 2022,” alisema Gavana Orengo.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
