“NI katika miaka miwili pekee ndani ya muongo uliopita ambapo Kenya imerekodi zaidi ya watoto 1.2 milioni waliozaliwa ndani ya kipindi cha miezi 12. Miaka hiyo ni 2021 na 2022. Kati ya miaka hiyo miwili, mwaka 2021 unashikilia rekodi kubwa zaidi kwa ongezeko la mwaka hadi mwaka la watoto wengi waliozaliwa. Kutoka watoto 1.13 milioni 1.13 waliozaliwa mwaka 2020, idadi hiyo iliongezeka kwa 73,428 na kufikia milioni 1.20 mwaka uliofuata. Uchambuzi wa ripoti za hali ya uchumi za Shirika la Taifa Kuhusu Takwimu Kenya (KNBS) kuanzia 2015 hadi 2025 unaonyesha kuwa mwaka 2022, watoto milioni 1.22 walizaliwa, ikiwa ni ongezeko la 21,254 kutoka mwaka uliotangulia. Ongezeko katika miaka ya 2021 na 2022 lilitokea wakati wa kafyu ya kudhibiti janga la Covid-19, ambapo shughuli nyingi za kijamii zilisimamishwa. Kesi ya kwanza ya Covid-19 nchini Kenya ilithibitishwa Machi 13, 2020. Siku mbili baadaye, Rais mstaafu Uhuru Kenyatta alitangaza hatua za awali za kudhibiti maambukizi, ikiwa ni pamoja na kufungwa kwa shule, kusitishwa kwa safari za kimataifa na marufuku ya mikutano ya kijamii. Mnamo Machi 25, 2020, serikali ilitangaza amri ya kutotoka nje usiku na baadaye ikazima kuingia na kutoka katika baadhi ya maeneo kama Nairobi na kaunti nyingine. Kwa kuzingatia ujauzito wa miezi tisa, watoto waliozaliwa kuanzia Januari 2021 walikuwa wa mimba za wakati wa kipindi cha mwisho wa Machi na Aprili 2020, wakati wa mwanzo wa hatua za kuzima Covid 19. Mhadhiri wa Saikolojia wa Chuo Kikuu cha Kenyatta, Dkt John Oteyo, anasema huenda sababu ni mbili: msongo wa mawazo na wanandoa kuwa na muda mwingi zaidi pamoja. Alieleza kuwa baadhi ya wanaume walitumia ngono kama njia ya kukabiliana na hofu ya janga hilo, akisema ilikuwa njia ya muda ya kujifariji wakati wa msukosuko. Pia alisema kufungwa kwa shughuli kulifanya wanandoa kuwa karibu zaidi, hivyo kuongeza uwezekano wa mimba.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
