skipToContent
🌐All

Familia ya Albert Ojwang bado yalilia haki mwaka mmoja tangu mauaji

Taifa Leo (Swahili) Global
Familia ya Albert Ojwang bado yalilia haki mwaka mmoja tangu mauaji
WAZAZI wa mwanamume aliyefia korokoroni sasa wanalilia haki wakilalamikia kutotimizwa kwa ahadi tele walizopewa na viongozi mbalimbali karibu mwaka mmoja tangu mwana wao alipokufa. Juni 7, 2025, waendeshaji pikipiki wawili waliwasili katika boma la Meshak Ojwang, katika kijiji cha Kakoth, Kabondo Kasipul, kupitia uani. Waliagizwa kumtwaa Albert Omondi Ojwang, 30, aliyeuawa siku mbili baadaye korokoroni alikozuiliwa kuhusiana na kuchapisha madai ya uongo dhidi ya Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Eliud Lagat. Nyumbani kwa Meshak, mabadiliko machache yamefanyika tangu mwanawe alipoaga dunia. Alipata nyumba mpya aliyojengewa kupitia usaidizi wa Gavana Gladys Wanga ambaye vilevile alikarabati nyumba (simba) ya mwanawe, Albert. Boma lao pia limewekwa ua, lango na tangi la kuhifadhi maji ya mvua. Kampuni ya stima iliunganisha nyumba ya Meshak na maboma yalizo jirani kupata umeme. Wakati wa maombolezi, watu wengi ikiwemo wanasiasa kama vile Rais William Ruto, marehemu Raila Odinga, na mashirika kadhaa yasiyo ya kiserikali, yaliahidi kusaidia familia hiyo. Hata hivyo, Meshak anasema ahadi nyingi hazijatimizwa. “Nakumbuka baadhi ya watu wakisema wanajiondoa kwa sababu tu nilimshukuru rais kwa kunisaidia wakati wa kuomboleza,” anasema. Anafafanua kwamba, kinyume na mbeleni ambapo angewasiliana na Albert, sasa hakuna mtu anayewea kumpa hela.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.