skipToContent
🌐All

Gen-Z wachambua Mswada wa Fedha 2026 kwa jicho la 2024

Taifa Leo (Swahili) Global
Gen-Z wachambua Mswada wa Fedha 2026 kwa jicho la 2024
KILICHOANZA kama midahalo kuhusu ushuru, kimegeuka kuwa moja kati ya vuguvugu bayana zaidi la kuelimisha raia kidijitali linaloongozwa na vijana wa Gen-Z, hali inayoibua kumbukumbu za Mswada wa Fedha wa 2024 uliosababisha maandamano kote nchini. Tangu wiki iliyopita, maelfu ya vijana hao wameendesha kampeni kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo kama vile TikTok, X, WhatsApp, video za Instagram na Telegram. Wamekuwa wakisoma Mswada wa Fedha wakichambua vipengee vya ushuru, kusambaza linki za kushiriki na kuwasilisha maoni kupitia tovuti ya Bunge. “Hii inatuathiri sote,” iligeuka mkarara. Mchakato wa kushirikisha umma mwaka huu umeshuhudia wimbi lisilotarajiwa la uhamasishaji kwenye mitandao. Miongoni mwa wanaohamasisha raia mitandaoni ni Allans Ademba, mwanzilishi wa mpango wa TUKO KADI ambaye Jumatatu alichapisha linki ya kushirikisha umma akihimiza Wakenya kujifahamisha kuhusu mapendekezo kwenye mswada. “Ushirikishaji wa umma kuhusu Mswada wa Fedha unakamilika leo 2026/2027,” alichapisha Ademba kwenye X. Miongoni mwa mapendekezo yaliyopingwa mno ni ushuru wa asilimia 25 kwa simu, ambao vijana wengi wanahofia utafanya simu, ukarabati na nyenzo za kidijitali kuwa ghali zaidi. Wengine wamepinga pendekezo la kutoza biashara kidijitali ushuru wa asilimia tano wakihoji kwamba waundaji matini tayari wanakabiliwa na sintofahamu kuhusu mapato na gharama ghali ya uundaji matini. Kinyume cha michakato ya kushirikisha umma inayohusishwa na mikutano ya hadhara, vikao vya vyombo vya habari au baraza, shughuli hii ilifanyika mitandaoni ikiendeshwa na Gen-Z waliojihami kwa simu, heshitegi na safu za kuelimisha raia mitandaoni. Walitafsiri istilahi ngumu katika lugha rahisi na kufafanua jinsi ada za ushuru zilizopendekezwa zitakavyowaathiri raia.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.