“W ATAFITI wamebaini kuwa kuanza siku kwa kushiriki mapenzi huimarisha hisia na motisha ya kuchapa kazi. Utafiti huo uliofanyika Amerika na kuchapishwa na jarida la New York Post , unasema kuwa na mnato wa hisia na mpenzi asubuhi husababisha utulivu. Pia wapenzi hupata motisha ya kuchapa kazi na kumakinikia kazi yao kuhakikisha kila kitu kinatekelezwa ipasavyo. Mapenzi nyakati za asubuhi husababisha kuachiliwa kwa homoni za oxytocin na dopamine. Homoni hizi huhusishwa na furaha, kupungua kwa msongo wa mawazo na kuwa na mlahaka mzuri. Wakati ambapo msongo wa mawazo upo chini na hisia kupanda, ni rahisi sana kwa mtu kumakinikia majukumu yake, kufanya maamuzi yenye hekima na kujukumika kwa umakinifu zaidi. Utafiti huo pia ulibaini kuwa si mapenzi pekee, bali pia kuzungumza asubuhi, kucheka na kuchangamkiana asubuhi husababisha siku yote kuwa ya furaha. Kutokana na kuimarika kwa uchapakazi, wanaoshiriki mapenzi asubuhi hupandishwa vyeo haraka kwenye taaluma zao. “Asilimia 71 ya wafanyakazi wote walioajiriwa walichapa kazi kwa asilimia 71, walitimiza makataa ya kazi kwa asilimia 70, umakanifu wao ulikuwa asilimia 58, motisha ya asilimia 57 na asilimia 54 waliridhia uchapakazi wao,” watafiti kutoka Shirika la Afya la ZipHealth wakafichua. Wamiliki wa biashara kubwa, wakurugenzi ndio wana uwezo wa kushiriki mapenzi asubuhi kwa asilimia 26, wakuu wa idara kwa asilimia 23 kisha waajiriwa wa kawaida kwa asilimia 16 sawa na wale ambao wameajiriwa na ndio wanaanza kazi. “Wale ambao hushiriki ngono asubuhi pia huwa wamefurahi sana, wanajiamini na hisia zao huwa dhabiti,” ukasema utafiti huo.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
