“RAIS William Ruto mnamo Jumamosi jioni alifanya ziara ya ghafla jijini Nairobi kukagua barabara na taa kabla ya Kongamano la Afrika linaloanza leo jijini Nairobi. Kiongozi wa nchi aliandamana na Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja, Waziri wa Barabara Davies Chirchir na Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wah. Rais alikagua miundomsingi ambayo ujenzi wake unaendelea viungani mwa jiji la Nairobi, maeneo ya kutembea na kuendesha baiskeli, jinsi mabomba ya kupitisha majitaka yanavyojengwa na miradi mingine. Kuzuru jiji kunakuja miezi michache baada ya Rais na Bw Sakaja kutia saini mkataba wa Sh80 bilioni mnamo Februari 17. Mkataba huo unalenga kuboresha miundomsingi, nyumba na miradi ya mazingira ambayo yanalenga kubadilisha jiji. Mnamo Aprili 9, Rais Ruto alihutubia Bunge la Kaunti ya Nairobi ambapo aliweka wazi kuwa halengi kutwaa majukumu ya serikali ya Bw Sakaja.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
