“Maafisa wakuu wa polisi na wizara ya elimu wanaelekea shule ya wasichana ya Utumishi Academy Gilgil ambako moto ulizuka usiku wa kuamkia Alhamisi, Msaidizi wa Naibu Inspekta Jenerali wa polisi, Masoud Mwinyi amesema. Alisema maafisa wa polisi pamoja na wachunguzi kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) walitumwa katika shule hiyo mara moja baada ya mkasa wa moto katika bweni kuripotiwa huku mamlaka zikianza zoezi la kuhesabu wanafunzi waliokuwapo wakati moto huo ulipozuka. Wazazi walifurika katika lango la shule hiyo kwa idadi kubwa baada ya habari za mkasa huo kusambaa kote Gilgil na maeneo jirani, huku polisi wakizuia watu wasiokuwa wazazi kuingia shuleni wakati uchunguzi na shughuli za uokoaji zikiendelea. Bw Mwinyi amesema ni wazazi pekee watakaoruhusiwa kuingia katika shule hiyo wakati maafisa wakikamilisha zoezi la kuhesabu wanafunzi. Bw Mwinyi amesema maafisa wakuu wa polisi na wizara ya elimu wanaelekea shuleni humo. “Tumepeleka maafisa wetu pamoja na wachunguzi wa DCI shuleni humo na kwa sasa zoezi la kuhesabu wanafunzi linaendelea ili kubaini idadi kamili ya waliokuwapo wakati moto ulipozuka. Kwa sasa, ni wazazi pekee watakaoruhusiwa kuingia shuleni,” alisema Munyi.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
