“RAIS William Ruto leo, Jumatatu, Juni 1, 2026 anaongoza taifa kuadhimisha miaka 63 ya Kenya kujitawala kutoka mikononi mwa mbeberu. Miongo sita na miaka mitatu iliyopita, Jamhuri ya Kenya ilipata uhuru wa ndani kwa ndani kujitawala chini ya Rais wa Kwanza hayati Mzee Jomo Kenyatta, ambaye kwa ushirikiano na vuguvugu la MauMau waliondoa utawala wa Muingereza. Wakati huo, Juni 1, 1963, Mzee Jomo Kenyatta ambaye ni babake Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, alihudumu kama Waziri Mkuu. Maadhimisho ya miaka 63 yanafanyika katika uwanja wa Wajir, yakiongozwa na Rais Ruto, aliyeandamana pia na naibu wake Prof Kithure Kindiki na viongozi wengine wakuu serikalini. Hufanyika kila mwaka Juni 1. Zifuatazo ni picha za hafla hiyo inayoendelea; [caption id="attachment_188696" align="aligncenter" width="300"] Rais Ruto akikagua gwaride la heshima. Picha|Manase Otsialo[/caption] [caption id="attachment_188697" align="aligncenter" width="300"] Pikipiki zinazoongoza msafara wa Rais. Picha|Manase Otsialo[/caption] [caption id="attachment_188698" align="aligncenter" width="300"] Rais William Ruto akisimama wima kwa heshima ya Madaraka Dei 2026. Picha|Manase Otsialo[/caption] [caption id="attachment_188699" align="aligncenter" width="300"] Bendi ya wanajeshi. Picha|Manase Otsialo[/caption] [caption id="attachment_188700" align="aligncenter" width="300"] Kikosi cha GSU kikiondoka uwanjani Wajir. Picha|Manase Otsialo[/caption] [caption id="attachment_188701" align="aligncenter" width="300"] Gwaride la wanajeshi. Picha|Manase Otsialo[/caption] [caption id="attachment_188702" align="aligncenter" width="300"] Usalama umeimarishwa Wajir Stadium. Picha|Manase Otsialo[/caption] [caption id="attachment_188704" align="aligncenter" width="300"] Wanafunzi wanaskauti wakati wa maadhimisho ya Madaraka Dei 2026. Picha|Manase Otsialo[/caption] [caption id="attachment_188705" align="aligncenter" width="300"] Umati wa wananchi waliojitokeza Wajir Stadium kuadhimisha Madaraka Dei 2026. Picha|Manase Otsialo[/caption] [caption id="attachment_188706" align="aligncenter" width="300"] Wanajeshi wakimpigia Rais William Ruto saluti. Picha|Manase Otsialo[/caption]
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
