skipToContent
🌐All

MAONI: Siasa za Magharibi kwa sasa ni mtihani mgumu kwa Ruto

MAONI: Siasa za Magharibi kwa sasa ni mtihani mgumu kwa Ruto
IKIWA kuna mwanasiasa aliyetumia mbinu bunifu kupenya katika siasa za magharibi katika uchaguzi mkuu uliopita alikuwa William Ruto ambaye alikuwa mgombea wa UDA. Inasemekana kutoka atika pembe tofauti kuwa kaunti ya Bungoma ndiyo iliyomsaidia Ruto kuwa Rais wa tano. Ili kuonyesha shukrani zake akamtuku Moses Wetangula kuwa spika wa bunge la taifa huku Musalia Mudavadi akifanywa mkuu wa mawaziri. Hata hivyo eneo hilo linaonekana kuwa na uasi mkubwa kutokana na nguvu changa za Linda Mwananchi ambayo ni merikebu ya seneta wa Nairobi Edwin Sifuna. Pili gavana wa Trans Nzoia George Natembeya ana vuguvugu lake la “Tawe” ambalo halitaki kusikia habari za UDA. Spika wa bunge Moses Wetangula amekuwa na mikutano kuwashwishi wakazi kuunga mkono juhudi za Rais Ruto kupewa muhula wa pili japo kuna upinzani mkubwa. Katika kaunti ya Kakamega ambako Rais katika serikali jumuishi alimpa kazi Wycliffe Oparanya kuwa waziri wake wa vyama vya ushirika na ustawi wa biashara ndogondogo, gavana huyo wa zamani wa Kakamega amesema kuwa mzozo katika ODM unawapa yeye na wenzake kazi ngumu mno kumwombea Rais kura. Kufikia hapo ni kaunti tatu kati ya tano ambapo upinzani umemega kwa kiasi fulani. Katika kaunti jirani ya Vihiga anakotoka Musalia Mudavadi uwanja wa Rais Ruto ni legevu kwa sababu kadhaa. Kwanza ODM ilimtimua seneta Godfrey Osotsi kuwa mmoja wa manaibu viongozi wa ODM. Osotsi anatoka katika kaunti hiyo na baadhi ya wakazi waliona kuwa alionewa na pia serikali haijawakamatwa waliomshambulia akiwa Kisumu. Mkutano wa Linda mwananchi uliokuwa Vihiga ulidhihirisha kuwa baadhi ya wakazi walikuwa na uchungu na serikali. Serikali ni UDA na sehemu ya ODM maarufu kama Linda ground. Katika mkutano uliofanya Jumapili iliyopita katika eneo bunge la Bumula na kuongozwa na gavana wa Trans Nzoia George Natembeya, watu walijaaa kama mchanga wa bahari. Natembeya aliposimama alisisitiza kuwa jamii ya waluhya itashirikiana licha ya kuwa katika mirengo tofauti ya upinzani yaani ule wa Sifuna wa linda mwananchi na ule waliomo Natembaya na washirika wa umoja wa upinzani. Hili la upinzani kusema watakaa pamoja linatakiwa limtie wasiwasi Rais William Ruto. Ikiwa ni kuwatafuta washiriki wengine afanye hivyo kwa dharura kwa sababu inavyoonekana meli za Wetangula na Mudavadi inaendelea kuzama katika bahari ya siasa za magharibi. Hata Busia hali si hali kwa UDA licha ya gavana Otuoma kuwataka wenyeji wampigie kura Ruto. Paul Nabiswa ni mhariri, NTV
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.