“ISLAMAD, Pakistan: AMERIKA na Iran jana zilikuwa zikikaribia kutia saini mkataba wa amani wa kuzima vita kabisa kati yao, duru ziliarifu. Makubaliano hayo yatasitisha vita lakini baadhi ya masuala tata bado hayatakuwa yameshughulikiwa vilivyo. Amerika na Iran zina uhasama mkali na pia msimamo mgumu ambao unaonyesha mkataba utakaoafikiwa utakuwa tu wa muda na huenda usiwe na mashiko jinsi inavyotarajiwa. Baada ya Iran kukalia ngumu mpango wake wa nyuklia na udhibiti wa mkondo wa Strait of Hormuz, Amerika inaonekana sasa imelegeza kamba huku ikimakinikia makubaliano yoyote ambayo yanalenga kusitisha vita. “Lengo letu ni kuhakikisha kuwa vita vinaisha kabisa kisha masuala mengine yataangaziwa kwenye mazungumzo yatakayofuata,” akasema afisa mmoja wa ngazi ya juu kutoka serikali ya Pakistani. Nchi hiyo imekuwa ikiongoza juhudi za upatanishi na afisa huyo alisema baada ya mkataba wa sasa kuafikiwa na kutiwa saini, kutakuwa na mazungumzo siku 30 zaidi kuhusu masuala tata. Rais wa Amerika Donald Trump alisema kuwa yupo tayari kwa maridhiano tangu vita hivyo vianze mnamo Februari 28. “Wanataka tuwe na mkataba na ni jambo ambalo linawezekana. Hivi vita vitaisha haraka sana,” akasema Trump. Pendekezo la kumaliza vita litakuwa pigo kwa matakwa ya Amerika kuwa Iran isitishe mpango wake wa nyuklia na pia ifungue mkondo wa Strait of Hormuz. Iran hata hivyo inaonekana imeanza kutilia shaka na haijaridhia pendekezo hilo, ikisema linajumuisha mengi ya matakwa ya Amerika. Spika wa Bunge la Iran Mohamed Baqer Qalibaf, alionekana kukejeli ripoti kuwa pande hizo mbili zilikuwa zikikaribia kupatana.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
