skipToContent
🌐All policy

Mauritius ‘yashangaa’ kusoma habari Trump anapanga kununua visiwa vyake

Taifa Leo (Swahili) Global
Mauritius ‘yashangaa’ kusoma habari Trump anapanga kununua visiwa vyake
CHAGOS, Mauritius MAURITIUS imethibitisha kuwa haijapokea pendekezo lolote kutoka kwa utawala wa Rais Donald Trump kuhusu ununuzi wa Visiwa vya Chagos. Hii ni baada ya gazeti la Telegraph kuripoti kwamba Ikulu ya White House ilikuwa ikitathmini mpango wa kuvinunua visiwa hivyo kutoka Mauritius. Katika taarifa yake, serikali ya Mauritius ilisema imeona yaliyochapishwa kwenye Telegraph . Hata hivyo ilisema bado haijawasilishiwa pendekezo rasmi wala kuwasiliana na Amerika, moja kwa moja au kwa njia nyingine kuhusu ununuzi wa Diego Garcia na Visiwa vya Chagos. “Msimamo wa Mauritius haujabadilika. Mamlaka yetu juu ya Visiwa vya Chagos hayawezi kujadiliwa,” ilisema serikali hiyo. Gazeti la Telegraph liliripoti Jumapili kuwa mpango wa ununuzi huo ulijadiliwa White House. Hii ni baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer kukabidhi mamlaka ya visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi kwa Mauritius.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.