“TAKRIBAN wanafunzi 15 wameripotiwa kufariki katika mkasa wa moto uliotokea katika shule ya Utumishi Girls iliyoko Gilgil, Kaunti ya Nakuru. Ripoti ya polisi inasema kwamba moto huo uliripotiwa saa saba za usiku katika bweni la wanafunzi 220 wa Gredi ya 10, Kidato cha Tatu na Kidato cha Nne. Inasema juhudi za kuzima moto zilizoongozwa na zimamoto wa Naivasha, KDF, Idara ya Misitu na NYS zilisaidia kukabili moto huo ingawa tayari maafa yalikuwa yametokea huku idadi isiyojulikana ya waliojeruhiwa wakikimbizwa katika hospitali mbali mbali. Viongozi wa ngazi za juu serikali akiwemo Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen, Waziri wa Elimu Julius Ogamba, Katibu wa Elimu Julius Bitok, Mkuu wa DCI Mohamed Amin, Naibu Mkuu wa Polisi Eliud Lagat na Kamati ya Bunge kuhusu Elimu wamefika shuleni humo kutathmini hali ambapo wanatarajiwa kutoa taarifa baadaye. Habari zaidi ni kadiri tunavyozipokea…
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
