“MTWAPA, Kilifi: MKE wa pasta mmoja mjini hapa hivi majuzi alimpiga breki demu muumini aliyezoea kumkumbatia mumewe. Demu huyo amekuwa akidai ni kwa kumpiga pasta pambaja ndipo hujihisi kupokea nguvu mpya za kiroho. Ni tabia ambayo imemkeketa maini mke wa pasta kwa muda mrefu hadi akaamua kuikomesha. Punde alipozima jaribio la demu kumfikia pasta hakutosheka, kwani ibada ilipofika tamati alisimama mbele ya kanisa na kutangaza paruwanja kwamba ni mwiko kwa demu yeyote kumpiga pambaja mumewe. “Wale mademu wanaotafuta roho kwa kumkumbatia bwanangu basi kuanzia leo kaeni bila roho. Sitakubali mchezo huo kwa mume wangu hata kama ni pasta wenu. Huyu ni baba wa watoto wangu. Tuheshimiane,” akafoka mama huyo.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
