skipToContent
🌐All

Murkomen atangaza Jumatano sikukuu ya Idd-ul-Adha

Murkomen atangaza Jumatano sikukuu ya Idd-ul-Adha
WAZIRI wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen ametangaza Jumatano kama sikukuu ya kitaifa. Kupitia notisi ya gazeti iliyochapishwa Jumatatu Mei 25, waziri huyo alitangaza kuwa siku hiyo ni ya Eid-ul-Adha ama sikukuu ya kuchinja kwa Waislamu. Eid-ul-Adha maarufu kama Iddi huadhimisha katika siku ya 10 ya Dhul Hijjah baada ya mahujaji kukamilisha ziara ya kidini ya Hajj, Mecca, Saudi Arabia. Siku hiyo huamuliwa kutokana na mwaandamo wa mwezi na kwa wasioenda Hajj, siku 10 za Dhul Hajj huwa ni za kufunga. “Kutokana na mamlaka ya Sheria za Sikukuu za Kitaifa, Waziri wa Usalama wa Ndani anatangaza kuwa Jumatano Mei 27 itakuwa sikukuu ya kitaifa kuadhimisha Eid-ul-Adha,” ikasema notisi hiyo ya gazeti. Eid-ul-Adha ni tofauti na Eid-ul-fitr ambayo huashiria mwisho wa mfungo wa Ramadhan. Siku hii ni ya kuadhimisha jinsi Mwenyezi Mungu alimwonea Ibrahimu imani na kumpa kondoo wa kiume achinje badala mwanawe Ishmael. Wanyama wenye kuchinjwa ni mbuzi, kondoo, ng’ombe na ngamia pekee. Ngamia na ngome wanasimamia watu saba (mnaweza kuchangisha watu saba kumnunua) kisha mbuzi na kondoo ni mtu mmoja. Mnyama anayechinjwa hafai kuwa na ulemavu wowote na nyama yake hugawanywa sehemu tatu ambazo ni chakula cha nyumbani (wewe na familia yako), kisha sehemu ya pili maskini na fukara na sehemu ya tatu ni majirani.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.