skipToContent
🌐All

Ndege yapasuka gurudumu na kuanguka ndani ya Maasai Mara

Ndege yapasuka gurudumu na kuanguka ndani ya Maasai Mara
NDEGE ilianguka Jumatatu, Juni 1, 2026 katika Mbuga ya wanyama ya Olkiombo, Maasai Mara japo hakuna ripoti kuhusu yeyote aliyeaga katika tukio lenyewe. Kamanda wa Polisi wa Narok Patrick Laboloa alithibitisha kuanguka kwa ndege hiyo saa sita mchana. Bw Lobola alikuwa ameahidi kuwa angetoa ripoti ya kina kuhusu ajali hiyo baadaye hapo jana. “Ndege hiyo ilianguka baada ya kupaa kutoka njia yake, gurudumu lake lilipopasuka,” duru ikaarifu Taifa Leo . Ndege hiyo ilikuwa imewabeba watalii kutoka Nairobi kuelekea Maasai Mara. Bado haikuwa imejulikana idadi ya abiria waliokuwa ndani. Polisi na uongozi wa Narok hawakuwa wamejibu jumbe na simu kuhusu kisa hicho huku ikisema walikuwa katika sherehe za Madaraka Dei.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.