skipToContent
🌐All

NMG yang’aa AMEA, yashinda tuzo sita za uandishi bora

NMG yang’aa AMEA, yashinda tuzo sita za uandishi bora
SHIRIKA la Habari la Nation Media Group (NMG) lilibuka mshindi katika makundi sita kwenye Tuzo za 14 za Vyombo vya Habari (AMEA) zilizofanyika Ijumaa usiku jijini Nairobi, likiendelea kuonyesha ubabe wake katika uandishi wa habari za upekuzi na maendeleo. Aidha, wanahabari wa NMG waliingia katika nafasi tatu bora katika makundi 14 tofauti, hali inayoendeleza historia ya mafanikio ya shirika hilo kubwa la habari nchini. Gazeti la Daily Nation pia lilitangazwa kuwa gazeti linalosomwa zaidi nchini Kenya. Mhariri Mkuu wa NMG, Dkt Joe Ageyo, aliwapongeza washindi hao akisema tuzo hizo ni thibitisho la uandishi wa habari unaozingatia maslahi ya umma ambao shirika hilo limekumbatia kwa zaidi ya miaka 60. Katika uandishi wa upekuzi, Jackline Macharia alishinda tuzo kwa makala ya “Brothers in Arms” iliyofichua mtandao wa biashara ya silaha kati ya Kenya na Sudan, huku Duncan Khaemba wa NTV akiwa mshindi wa pili kwa makala kuhusu ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines ya mwaka 2019. Katika kipengele cha utawala na maendeleo, Ruth Chesenge alishinda kwa makala yake “Blood Gold” iliyohusu migogoro ya madini katika eneo la Ikolomani, Kakamega. Kwa upande wa jinsia na ujumuishi, Moraa Obiria alituzwa kwa makala yake “Broken Boys, Broken Men” iliyochambua changamoto za kisaikolojia kwa wanaume. Katika uandishi wa michezo, Dominic Maichuhie alishinda kwa makala kuhusu unyanyasaji wa kijinsia katika kambi ya mazoezi ya wanariadha. Katika utalii, Sinda Matiko alishinda kwa uchambuzi wa mabadiliko ya ajira katika sekta ya hoteli na safari za meli za kimataifa. Waandishi wengine wa NMG pia waliibuka washindi wa pili na watatu katika makundi mbalimbali yakiwemo elimu, biashara, afya, mazingira, picha na video. Dkt Ageyo alisema tuzo hizo zinaonyesha kuwa licha ya changamoto za kidijitali na kiuchumi, uandishi wa habari wa upekuzi na unaolenga jamii bado una nafasi kubwa nchini Kenya.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.