skipToContent
🌐All

Nyong’o ajitambulisha na mrengo wa Tutam

Nyong’o  ajitambulisha na mrengo wa Tutam
GAVANA wa Kisumu Profesa Anyang’ Nyongó jana alijitokeza hadharani na kujihusisha na mrengo wa ODM unaogemea Seneta wa Siaya Dkt Oburu Oginga huku akitoa wito wa umoja wa chama. Jana, jamii ya Waluo ilikongamana Kisumu ambapo kwa kauli moja ilitangaza kuwa inamuunga mkono Rais William Ruto achaguliwe kwa muhula wa pili. Profesa Nyongó alimkaribisha Dkt Oginga na viongozi wengine ambao aliwaambia kuwa wanastahili kufahamu ODM si chama cha eneo hilo pekee. Alisisitiza kuwa ataunga mkono kile ambacho kinazingatia maslahi ya wananchi na kupinga kile kinachowakandamiza. Gavana huyo alisema kuwa njia ya kumuenzi marehemu kigogo wa chama hicho Raila Odinga si kutaja jina lake katika kila mazungumzo bali kusimamia falsafa yake.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.