“UJENZI wa mradi wa bwawa la Mwache wa Sh20 bilioni unakabiliwa na matatizo ya kifedha ambayo yanahatarisha kukwamisha kukamilika kwa mradi huo kwa wakati uliopangwa. Bwawa hilo lenye kina cha mita 84 na ambalo linatarajiwa kuhifadhi zaidi ya mita milioni 127 za maji, linaendelea kwa kasi ya chini zaidi na linaweza kusimama iwapo serikali haitatoa Sh1.9 bilioni kwa ajili ya fidia na kazi nyinginezo. Wanachama wa Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Maji, Umwagiliaji na Uchumi wa Bahari walieleza hofu kuhusu kucheleweshwa kwa mradi huo, lakini wakaendelea kuwa na matumaini kuwa Hazina ya Taifa itatoa fedha zilizotengwa kwa ajili ya mradi huo. [caption id="attachment_188004" align="alignnone" width="2000"] Rais William Ruto wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Bwawa la Mwache, Kwale, Aprili 6, 2023. Bwawa hili lilitarajiwa kukamilika ndani ya miezi 36. Picha|Maktaba[/caption] Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw Kangogo Bowen, alisema serikali imetenga Sh52.8 bilioni kwa mwaka wa kifedha wa 2026/2027 kusaidia mradi huo. “Tuna matumaini kuwa fedha za mwaka ujao wa kifedha zitatolewa kama ilivyopangwa na kwa wakati ufaao, kwani ucheleweshaji wowote utakwamisha mradi huu kabisa,” alisema Bw Bowen. Bw Bowen alisema fedha hizo zitasaidia kukamilisha ujenzi wa mtambo wa kusafisha maji pamoja na uwekaji wa mabomba ya usambazaji maji. Kamati hiyo wakati wa ziara yake ilithibitisha kuwa kampuni ya Sinohydro Corporation Limited inayotekeleza mradi huo imeripoti kupungua kwa kasi ya kazi kutokana na madeni ambayo hayajalipwa ya kiasi cha Sh1.9 bilioni. Mradi wa bwawa la Mwache ambao kwa sasa umefikia asilimia 83 unatarajiwa kuongeza usambazaji wa maji kwa Mombasa ambayo kwa sasa ina upungufu wa asilimia 75, na pia utatoa maji ya umwagiliaji kwa zaidi ya ekari 6,000 kwa wakulima wa Kwale.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
