skipToContent
🌐All

Pigo kwa Gachagua, korti yatupilia mbali kesi ya kutimuliwa serikalini, yamliwaza na Sh50m

Taifa Leo (Swahili) Global
Pigo kwa Gachagua, korti yatupilia mbali kesi ya kutimuliwa serikalini, yamliwaza na Sh50m
ALIYEKUWA Naibu Rais Rigathi Gachagua amepata pigo kubwa mahakamani, baada ya jopo la majaji watatu kutupilia mbali kesi ya kupinga kutimuliwa kwake serikalini. Katika uamuzi wa majaji Fridah Mugambi, John Mrima na Eric Ogola, walisema kwamba sheria zilifuatwa katika mchakato mzima wa kumtimua Bw Gachagua uongozini. Jopo hilo, hata hivyo, lilisema mahali pekee Seneti ilipokosea ni kutompa nafasi ya kujitetea kibinafsi, haswa wakati alipougua na kukimbizwa katika hospitali ya Karen. Na kwa hilo, majaji wameafikia kumtunuku Sh50 milioni kama kiliwazo. Mahakama ilikuwa imeorodhesha malilio sita ya Gachagua ambayo mawakili wake waliwasilisha wakitaka uamuzi bayana kuyahusu. Nayo yalikuwa iwapo Mahakama Kuu ilikuwa na uwezo wa kisheria kusikiza kesi yake, kwamba kulikuwa na uonevu dhidi yake, iwapo umma ulihusishwa katika kutoa maoni, uhalali wa kanuni za bunge zilizotumiwa katika mchakato wa kumtimua, ufaafu wa Kithure Kindiki kuchukua wadhifa wake na iwapo Katiba ilifuatwa katika kumtimua. Kuhusu kigezo cha uonevu na kutopewa nafasi ya kusikizwa, jopo la majaji watatu lilisema kukiukwa kwa haki hiyo hakuwezi kutumiwa kuharamisha kutimuliwa kwake. Pia majaji hao walisema kuwa kumrejesha madarakani kutasababisha kuwe na manaibu rais wawili jambo ambalo haliwezani kisheria. Ingawa hivyo, mawakili wa Bw Gachagua wakiongozwa na Paul Muite wamesema kuwa watakata rufaa kuhusu uamuzi huo.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.