“TUDOR, Mombasa VIJANA wa kanisa moja mtaani hapa walimwacha pasta wao akichana mbuga huku anapiga nduru, walipopanga kisanga cha kujaribu imani yake. Kila Jumapili pasta amekuwa akihimiza waumini wasiache imani hata wakikabiliwa na vitisho au mateso. Mahubiri yalipokuwa yakiendelea ghafla vijana 10 waliovaa vitambaa usoni waliingia kanisani na kutangaza wao ni genge la wahalifu. Waumini waliingiwa na hofu wakamtazama pasta. Alipoona hatari ikiwakodolea macho pasta aliruka kutoka jukwaani na kutimua mbio hadi nje akipiga mayowe akiomba msaada. Baada ya muda mchache vijana hao walivua vitambaa na kuanza kucheka. “Msihofu, sisi ni vijana wa kanisa hili. Tulitaka tu kupima kama pasta anaishi kulingana na mahubiri yake,” walitangaza huku waumini wakibaki mdomo wazi wamepigwa na butwaa.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
