skipToContent
🌐All

Rapa Octopizzo amejitosa kugombea ubunge wa Kibra 2027, asisitiza hatafuti utajiri

Taifa Leo (Swahili) Global
Rapa Octopizzo amejitosa kugombea ubunge wa Kibra 2027, asisitiza hatafuti utajiri
MWANAMUZIKI na mjasiriamali Henry Ohanga maarufu Octopizzo anasema kama ni utajiri tayari ameshafanikiwa kuwa nao, hivyo azma yake ya kugombea ubunge wa Kibra mwaka ujao inatokana na dhamira kubwa ya kusaidia jamii. “Kama ni utajiri tulishafanikiwa kitambo. Maisha yangu yote nimelelewa na kuishi Kibra, naelewa magumu wanayopitia watu. Nimekuwa nikijitahidi sana kubadilisha maisha ya wakazi wa Kibra kupitia wakfu wangu wa Octopizzo Foundation,” alisema. “Ila nimefikia sehemu nikahisi kwamba nikiwa mbunge wa eneo hili nitapata fursa na jukwaa la kusaidia watu wengi zaidi. Madhumuni yangu ni kuona maisha ya watu wa mtaa niliozaliwa yakibadilika,” akaeleza msanii huyo aliyezaliwa na kulelewa katika mtaa huo wa mabanda. Akiongeza kutetea uamuzi wake wa kujitosa kwenye siasa alihoji kwamba kuwa sehemu ya muziki wake huangazia siasa, hasa suala la kutetea jamii na kusuta sera mbovu za serikali.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.