skipToContent
🌐All

Ruku afokea Gachagua kwa kutaka wakazi Mlimani ‘wamsikilize Ruto na wamwache aende’

Ruku afokea Gachagua kwa kutaka wakazi Mlimani ‘wamsikilize Ruto na wamwache aende’
WAZIRI wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku amemshambulia vikali aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, akisema kuwa Rais William Ruto hahitaji ruhusa wala baraka za mtu yeyote kutembelea na kuzindua miradi ya maendeleo eneo la Mlima Kenya. Akizungumza wakati wa ibada ya kanisa la NICA mjini Embu, Bw Ruku alipuuza kauli ya Bw Gachagua kuwataka wakazi wa Mlima Kenya “wamsikilize Rais Ruto na wamwache aende,” akizitaja kuwa za kupotosha na zisizo na uwajibikaji. Bw Ruku alisema kuwa Rais ni kiongozi wa kitaifa aliyechaguliwa na Wakenya wote, hivyo ana haki na wajibu wa kutembelea sehemu yoyote ya nchi bila vitisho au masharti kutoka kwa mtu yeyote. Alisisitiza kuwa hakuna kiongozi mmoja anayemiliki Mlima Kenya au mwenye mamlaka ya kuamua nani anaweza kuzungumza na wakazi wake. “Rais ana jukumu kubwa zaidi la kuwahudumia Wakenya wote kwa usawa. Hakuna sehemu yoyote ya nchi hii ambako hawezi kuenda kuzindua miradi na kukagua maendeleo,” akasema Bw Ruku. Waziri huyo pia alimlaumu Bw Gachagua kwa madai ya kujaribu kuwagawanya viongozi na jamii kupitia kampeni za mapema za kisiasa kuelekea kura ya 2027. Bw Ruku pia alipinga kauli za mara kwa mara za aliyekuwa naibu rais kwamba atawania urais mwaka 2027, akisema kuwa kiongozi aliyeondolewa madarakani na bunge hana nafasi kama hiyo. Aidha, Bw Ruku pia alimvamia Mbunge wa Manyatta, Gitonga Mukunji, akisema ameshindwa kuanzisha miradi kwa wananchi wa eneobunge lake huku akijihusisha na kampeni za mapema za ugavana wa Embu. “Uongozi hupimwa kwa utoaji wa huduma, si kwa kauli za kisiasa au umaarufu mitandaoni,” akasema.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.