“SENETI imetilia shaka ushahidi wa matibabu uliowasilishwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua katika kesi inayoendelea kuhusu kuondolewa kwake mamlakani. Kupitia Karani wa Seneti Jeremiah Nyegenye, Seneti pamoja na Spika Amason Kingi imehoji uhalali, muda na stakabadhi za hospitali zilizowasilishwa na daktari wa moyo Daniel Gikonyo. Seneti inasema rekodi hizo zina utata, zina mapungufu na hazikuwahi kuwasilishwa mbele ya maseneta wakati wa kusikizwa kwa kesi ya kumbandua Gachagua ofisini. Gachagua na walalamishi wengine 40 wanadai Seneti ilikiuka haki yake ya kusikizwa kwa haki kwa kuendelea na mchakato huo wakati alikuwa mgonjwa na kulazwa hospitalini. Dkt Gikonyo aliambia mahakama kuwa, Gachagua alilazwa Oktoba 17, 2024 akiwa na maumivu makali ya kifua yaliyohitaji matibabu ya dharura na uangalizi wa saa 48 hadi 72. Hata hivyo, Seneti sasa inasema ripoti ya hospitali inaonyesha Gachagua alilazwa Oktoba 17 na kuruhusiwa kuondoka Novemba 20, hali ambayo inaashiria alikaa hospitalini kwa siku 31. Seneti inasema muda huo unakinzana na maelezo ya daktari huyo na unafanya ushahidi huo kutiliwa shaka. Pia Seneti imehoji kwa nini mawakili wa Gachagua hawakuwasilisha stakabadhi hizo wakati wa kusikizwa kwa kesi licha ya kuahidi kufanya hivyo.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
