skipToContent
🌐All

Sikuwa na nia ya kudharau Waziri, ni vile tu nachukia uongo – Kaunda

Taifa Leo (Swahili) Global
Sikuwa na nia ya kudharau Waziri, ni vile tu nachukia uongo – Kaunda
KILICHOANZA kama maoni tofauti katika kikao cha mazungumzo sasa kimemgeuza Kennedy Kaunda kuwa gumzo nchini kutokana na maneno aliyotumia kumpinga Waziri wa Kawi Opiyo Wandayi akisema: “Kwa heshima zote.” Bw Kaunda alikuwa miongoni mwa wadau wa sekta ya usafiri wa umma walioalikwa katika mkutano wa dharura uliolenga kufuta mgomo wa matatu uliotikisa shughuli za kawaida katika miji mikuu Jumatatu hadi alfajiri ya siku iliyofuata. Alijitokeza kuzungumza muda mfupi baada ya Waziri wa Kawi Bw Wandayi na Waziri wa Uchukuzi Davis Chirchir kuzungumza na wanahabari baada ya kikao cha saa tano. Bw Wandayi alipotangaza kuwa serikali ilikuwa imepunguza bei ya dizeli kwa Sh10 na kushughulikia suala la kuchanganya mafuta katika vituo vya mafuta, wadau wa sekta ya usafiri walikuwa na msimamo tofauti. Akifahamu kuwa asingepata nafasi ya kuzungumza baada ya mawaziri kutoa taarifa yao, Bw Kaunda, ambaye ni mshiriki wa kanisa la SDA na mwimbaji wa kwaya, alitumia sauti yake nzito kuvutia wanahabari. “Kwa heshima zote,” alisema huku kamera zikimumlika. “Tulikubaliana kwamba tutakuwa wazi kwa umma kuwa hatujafikia makubaliano. Kitu pekee tulichokubaliana ni muda wa kutoka katika ukumbi wa mkutano,” alisema Bw Kaunda.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.