skipToContent
ChinaAll

Trump arai Rais Xi kushinikiza Iran ifungue Mkondo wa Hormuz

Trump  arai Rais Xi kushinikiza Iran ifungue Mkondo wa Hormuz
RAIS wa Amerika, Donald Trump, alisema kuwa Rais wa China, Xi Jinping, alikubali kwamba Tehran lazima ifungue tena Mkondo wa Bahari wa Hormuz, ingawa China haikutoa ishara yoyote kuwa ingeingilia kati suala hilo. Trump baada ya kukamilisha mazungumzo ya siku mbili na Xi kutoka Beijing, alisema kuwa iwapo Amerika itaondoa vikwazo dhidi ya kampuni za mafuta za China zinazouza mafuta kutoka Iran kwa kuwa China ndiyo mnunuzi mkubwa zaidi. “Siombi upendeleo wowote kwa sababu ukiomba ukifanya hivyo, lazima nawe urudishe mkono,” alisema Trump alipoulizwa na waandishi iwapo Xi alikuwa ameahidi rasmi kushinikiza Iran kufungua njia hiyo muhimu ya baharini. Hata hivyo Xi hakutoa maoni kuhusi mazungumzo yake na Trump kuhusu Iran, ingawa wizara ya mambo ya nje ya China ilieleza kutoridhishwa kwake na vita vya Iran, ikisema kuwa ni mzozo ambao haukupaswa kutokea na hauna sababu ya kuendelea. Iran ilifunga kwa kiasi kikubwa Mkondo wa Hormuz, ambao ulikuwa ukipitisha asilimia 20 ya mafuta na gesi asilia iliyoyeyushwa duniani kabla ya Amerika na Israeli kuanzisha mashambulizi mnamo Februari 28. Kuvurugika kwa usafirishaji huo kumesababisha mgogoro mkubwa zaidi wa usambazaji wa mafuta kuwahi kushuhudiwa, huku bei za mafuta zikipanda kwa kasi. Maelfu ya Wairani waliuawa wakati wa mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na serikali za Amerika na Israeli, huku maelfu wengine wakipoteza maisha nchini Lebanon kutokana na mapigano mapya kati ya Israeli na kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran. Amerika ilisimamisha mashambulizi yake mwezi uliopita lakini ikaendelea na kufunga bandari. Tehran ilisema haitafungua tena njia hiyo ya baharini hadi Amerikai itakapositisha mzingiro wake wa bandari. Trump ametishia kuanzisha tena mashambulizi ikiwa Iran haitaunga mkono makubaliano. “Tunahitaji njia za baharini zibaki wazi, na hatutaki wawe na silaha za nyuklia,” alisema Trump akiwa Beijing pamoja na Xi. Iran, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikikana kuwa na nia ya kutengeneza silaha za nyuklia, imekataa kusitisha utafiti wake wa nyuklia au kuachana na akiba yake ya siri ya urani iliyoongezwa nguvu, jambo ambalo limemkera Trump.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.