skipToContent
ChinaAll policy

Trump asema mazungumzo na Iran yanakaribia kusambaratika

Trump asema mazungumzo na Iran yanakaribia kusambaratika
WASHINGTON, Amerika: MATUMAINI ya kupatikana kwa muafaka kati ya Amerika na Iran yalididimia Jumanne baada ya Rais Donald Trump kusema mazungumzo yalikuwa yanaelekea kusambaratika. Hii ni baada ya Iran kukataa pendekezo la Amerika la kumaliza vita hivyo na kushikilia orodha ya matakwa yake ambayo lazima yatimizwe. Trump alikuwa amerejelea orodha hiyo kama ‘takataka’. Iran ilikuwa imependekeza mwisho wa vita hivyo ushirikishe hadi Lebanon ambako Israel, mshirika wa Amerika, inapambana na Kundi la Hezbollah. Aidha, Iran ilisisitiza kuwa mkondo wa mafuta wa Strait of Hormuz ni himaya yake wala haufai kuingiliwa na pia ikataka fidia kutokana na uharibifu wa mali na maafa yaliyotekelezwa na Amerika. Isitoshe, ilitaka Amerika iondoe meli zake ambazo zimezuia uchukuzi Pwani mwa Iran kati ya masharti mengine. Trump Jumanne alisema Iran haina nia ya kumalizwa kwa vita hivyo na mazungumzo hayo yaliyoanza Aprili 7 baada ya kusitishwa kwa vita, yananingínia padogo. Maafisa wa Iran nao wametoa kauli zinazoashiria kuendelea kuwa imara licha ya shinikizo za Amerika katika vita hivyo. Ripoti ya shirika la habari la Fars ilimnukuu Mohammad Akbarzadeh, naibu mkurugenzi wa masuala ya kisiasa wa Jeshi la Wanamaji la IRGC, akisema kuwa Iran imeongeza udhibiti wake wa Strait of Hormuzz na kuugeuza kuwa makao makuu ya oparesheni zake za kijeshi. Mnamo Jumatatu, Amerika iliweka vikwazo vipya dhidi ya watu binafsi na kampuni ilizodai zinasaidia Iran kusafirisha mafuta hadi China, kama sehemu ya juhudi za kuzuia ufadhili wa kijeshi na nyuklia kwa Iran. Haya yanajiri huku Trump akitarajiwa kuwasili Beijing leo, ambapo suala la Iran linatarajiwa kuwa miongoni mwa mada zitakazojadiliwa na Rais wa China Xi Jinping. Mzunguko wa meli kupitia Strait of Hormuz umepungua sana ikilinganishwa na hali ilivyokuwa kabla ya vita. Takwimu za usafirishaji kutoka kampuni za Kpler na LSEG zilionyesha kuwa meli tatu za mafuta ghafi zilivuka njia hiyo wiki iliyopita zikiwa zimezima vifaa vyao vya ufuatiliaji ili kuepuka kushambuliwa na Iran. Nchini Amerika, tafiti zinaonyesha kuwa vita hivyo havina uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa raia, ambao sasa wanakabiliwa na ongezeko la bei ya mafuta chini ya miezi sita kabla ya uchaguzi wa kitaifa. Uchaguzi huo utakaamua iwapo chama cha Republican cha Trump kitaendelea kudhibiti Bunge la Congress.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.