skipToContent
🌐All

Trump: Iran imenitii sasa sitaishambulia

Trump: Iran imenitii sasa sitaishambulia
WASHINGTON, Amerika: RAIS wa Amerika Donald Trump jana alisema kwamba amesitisha mashambulio yaliyokuwa yamepangwa dhidi ya Iran baada ya Tehran kuwasilisha pendekezo la amani kwa Washington. Trump anasema hatua ya Iran sasa ina maana kwamba kuna uwezekano mkubwa sana wa kuafikiwa kwa makubaliano ya kudhibiti mpango wa nyuklia wa Iran. Baada ya Iran kuwasilisha pendekezo jipya la amani kwa Amerika, Trump alisema ameliagiza jeshi la Amerika lisishambulie Iran mnamo Jumatano. Hata hivyo, anasema Iran itashambuliwa iwapo itaghairi nia na muafaka huo ukose kuafikiwa. Kauli ya Trump ilitolewa wakati ambapo hakukuwa na habari zozote ulimwenguni kuwa alikuwa akipanga kushambulia Iran na kuendeleza vita ambavyo vilianza mnamo February 28. Hapo awali Trump, alikuwa ameonyesha matumaini kwamba makubaliano ya kumaliza vita yalikuwa karibu kupatikana na pia akatishia kuishambulia Iran vikali ikiwa makubaliano hayangekwepo. Katika ujumbe wake, alisema viongozi wa Qatar, Saudi Arabia na Umoja wa Mmilki za Kiarabu walimwomba asitishe shambulizo hilo kwa sababu hatimaye kutakuwa na muafaka. Hata hivyo, hakutoa maelezo ya makubaliano hayo yanayojadiliwa. Akizungumza na waandishi wa habari baadaye, Trump alisema Amerika itaridhika ikiwa itafikia makubaliano na Iran ambayo yatazuia Tehran kupata silaha ya nyuklia. “Inaonekana kuna nafasi nzuri sana ya wao kuafikia suluhu. Ikiwa tunaweza kufanya hivyo bila kuwashambulia kwa mabomu makubwa, nitafurahi sana,” akasema Trump. Tangazo la Trump la kusitisha shambulizo hilo lilikuja baada ya msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, kuthibitisha kwamba matakwa yao yamewasilishiwa Amerika kupitia Pakistan. Duru kutoka Pakistan zilieleza kuwa imefikishia Amerika msimamo wa Iran ila pande zote bado zilikuwa zikishikilia msimamo mgumu. “Pande zote zinaendelea kushauriana hasa kuhusu masuala tata. Hatuna muda mwingi,” ikaarifu duru hizo. Haya yakiendelea, Iran nayo ilisisitiza kuwa haitatereka na iwapo Amerika inataka kuwashambulia, nao wapo tayari kulipiza kisasi. Makao makuu ya pamoja ya jeshi la Iran, Khatam al-Anbiya, yalisema vikosi vyao viko tayari kujibu mara moja mashambulizi ya Amerika. “Uvamizi au mashambulizi yoyote mapya yatajibiwa haraka tena kwa nguvu zaidi,” akasema Kamanda wa Khatam al-Anbiya, Ali Abdollahi.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.