“RAIS Mstaafu Uhuru Kenyatta ni kati ya viongozi waliowasili Uganda jana kwa hafla ya kuapishwa kwa Rais Yoweri Museveni leo. Kwenye chapisho katika ukurasa wake wa X, Bw Kenyatta alithibitisha kuwa amewasili Uganda na alipokelewa na maafisa wa ngazi ya juu wa serikali ya taifa hilo. Kati ya waliomlaki ni Balozi Katureebe Tayebwa na Baloz Kipkosgei Toroitich. Rais Museveni alichaguliwa tena kwa muhula wa saba mnamo Januari 15 na ataendelea kuongoza nchi hiyo tangu achukue usukani kwa mara ya kwanza mnamo 1986. Marais na viongozi kutoka mataifa mbalimbali Afrika na nje ya bara hili wanatarajiwa kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Museveni.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
