skipToContent
🌐All

Wanafunzi wahofiwa kufariki moto ukizuka katika bweni Utumishi Girls

Wanafunzi  wahofiwa kufariki moto ukizuka katika bweni Utumishi Girls
Wanafunzi kadhaa wanahofiwa kufariki dunia baada ya moto kuzuka katika bweni la shule ya Utumishi Girls Academy huko Gilgil, Kaunti ya Nakuru, alfajiri ya Alhamisi, hali iliyozua hofu na taharuki miongoni mwa wazazi, walimu na wakazi waliokusanyika nje ya shule hiyo. Ripoti zinaonyesha kuwa moto huo ulianza saa saba usiku, ingawa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya lilisema tukio hilo liliripotiwa rasmi majira ya saa tisa na nusu alfajiri huku vikosi vya dharura vikikimbia shuleni humo kudhibiti hali na kuwasaidia wanafunzi walioathirika. “Kufuatia tukio la moto lililoripotiwa majira ya saa tisa na nusu alfajiri katika shule ya Utumishi Girls Academy kaunti ya Nakuru, Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya liitikia kutoa msaada katika shughuli zinazoendelea za kukabiliana na dharura hiyo,” ilisema taarifa ya shirika hilo. Shirika hilo lilithibitisha kuwa maafisa wake wa usaidizi wa kisaikolojia walikuwa tayari wamewasili shuleni humo kusaidia wanafunzi, wazazi na walimu waliopatwa na mshtuko huku hali halisi ya mkasa huo ikiendelea kutatanisha wengi. “Wahudumu wetu wa kwanza, wahudumu wa ambulansi wa E-Plus pamoja na maafisa wa usaidizi wa kisaikolojia kwa sasa wako eneo la tukio wakitoa msaada kwa wanafunzi walioathirika pamoja na wahudumu wengine na mamlaka husika,” ilisema Msalaba Mwekundu Kenya.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.