“WATU wanne walijeruhiwa baada ya wafuasi wa Chama cha United Democratic Alliance (UDA) na Democracy for Citizens Party (DCP) kuvurugana katika uchaguzi mdogo wa Emurua Dikirr uliofanyika Alhamisi. Kwa mujibu wa polisi, tukio hilo lilitokea karibu na vituo vya kupigia kura vya Chelemei na Kiribwet katika wadi ya Kapsasian, ambapo waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali mbalimbali kupatiwa matibabu. Tukio hilo lilitokea wakati wapiga kura 44,457 wa eneo bunge la Emurua Dikirr, Kaunti ya Narok, walipokuwa wakiendelea kupiga kura kumchagua mrithi wa aliyekuwa Mbunge wa awamu tatu Johana Ngeno. Tume ya IEBC iliwaidhnisha wagombeaji David Kipsang Keter (UDA), Desma Cherono (PNU), Vincent Rotich (DCP), Gideon Koech (NVP) na Kenneth Kiprono (RLP). Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Narok Patrick Lobolia alithibitisha vurugu kati ya wafuasi wa UDA na DCP, huku wagombea wakitoa wito wa utulivu na kuimarishwa kwa usalama kuzuia kuongezeka kwa mvutano. Mmoja wa majeruhi alitibiwa katika hospitali ya Chebunyo katika Kaunti jirani ya Bomet, huku wengine wawili wakitibiwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Emurua Dikirr.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
