skipToContent
🌐All

Wito wa amani, gharama nafuu ya maisha watanda wakati wa Idd

Wito wa amani, gharama nafuu ya maisha watanda wakati wa Idd
VIONGOZI wa Kiislamu wamewataka wabunge wa Bunge la Kitaifa kuhakikisha bajeti ijayo inawapunguzia Wakenya makali ya maisha badala ya kuongeza mzigo wa ushuru. Wakizungumza wakati wa sherehe za Idd-Ul-Adha katika Shule ya Msingi ya Uasin Gishu mjini Eldoret, viongozi wa Kiislamu kutoka eneo la North Rift waliwaonya wanasiasa dhidi ya kupitisha bajeti inayopuuzilia mbali masaibu ya wananchi wanaokumbwa na gharama ya juu ya maisha kutokana na ushuru mkubwa wa mafuta. Wakiongozwa na Imam wa Msikiti wa Jamia Eldoret Hussein Mohammed, viongozi hao walisema wananchi wanahitaji afueni ya kiuchumi badala ya ushuru mpya utakaowaongezea mateso. Katika kaunti ya Trans Nzoia, waumini wa Kiislamu walikusanyika katika Msikiti wa Jamia mjini Kitale kusherehekea Idi al-Adha huku wakihimizwa kusaidiana, kuonyesha maskini huruma na kusameheana. Sherehe hizo ziliongozwa na Imam Ismail Bono Hajir ambaye aliwataka Waislamu kupendana na kusaidiana bila ubaguzi. Waumini hao pia waliitaka serikali kupunguza bei ya mafuta wakisema gharama ya maisha imewaathiri wananchi wengi. Wakati huo huo, mamia ya Waislamu katika kaunti ya Mombasa walikusanyika katika viwanja vya Tononoka na misikiti mbalimbali kuadhimisha Eid-ul-Adha huku viongozi wa dini na kisiasa wakitoa wito wa amani, mshikamano na kujitolea kwa taifa. Mwanachuo Zenu Noordin Ali Mohammed alisema sikukuu hiyo huwakumbusha Waislamu umuhimu wa utiifu kwa Mungu, kujitolea na kuwasaidia wahitaji. Katika uwanja wa Tononoka, mhubiri Abu Khatada aliwataka viongozi wa kisiasa kuepuka siasa za mgawanyiko na kuhubiri amani. Waziri wa Madini na Uchumi wa Bahari, Hassan Joho, alisema viongozi wanapaswa kuweka mbele maslahi ya wananchi na kushirikiana kwa maendeleo ya taifa. Kwa upande wake, katibu wa UDA Hassan Omar aliwataka Wakenya kudumisha umoja akisema serikali inalenga kuhudumia maeneo yote ya nchi kwa usawa.
Share
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Read full article

Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.