“HUKU Kenya ikitoa tahadhari kuhusu mlipuko wa Ebola unaoendelea nchini Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), maafisa wa afya wameanza kuimarisha maandalizi katika mipaka, viwanja vya ndege na hospitali ili kuzuia kuingia kwa ugonjwa huo nchini. Tahadhari hiyo inafuatia kuenea kwa aina ya ugonjwa huo ya Bundibugyo katika mataifa hayo mawili jirani. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Ebola ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vya familia ya Filoviridae. Ugonjwa huo ulitambuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1976 nchini Sudan Kusini na karibu na Mto Ebola nchini DRC. Kuna aina sita za virusi vya Ebola, lakini aina tatu ndizo zimehusishwa na milipuko mikubwa kwa binadamu. Mlipuko wa sasa unasababishwa na aina ya Bundibugyo ambayo hadi sasa haina chanjo wala tiba iliyoidhinishwa. WHO inaeleza kuwa kiwango cha vifo vya Ebola kinaweza kufikia asilimia 50, ingawa kwa aina ya Bundibugyo kiwango hicho huwa kati ya asilimia 25 hadi 50. Mtaalamu wa magonjwa kutoka Nairobi, Dkt Ahmed Kalebi, amesema changamoto kubwa ni kwamba wagonjwa wengi hawaonekani kuwa na Ebola katika hatua za mwanzo za maambukizi. “Mara nyingi hawaonyeshi dalili za kutokwa damu kama watu wengi wanavyodhani. Wanaweza kuonekana kama wana homa ya kawaida, malaria au maambukizi ya tumbo,” alisema. Virusi vya Ebola huenezwa pale mbapo mtu anatagusana moja kwa moja na damu au majimaji ya mwili wa mtu aliyeambukizwa. Ugonjwa huo pia unaweza kusambazwa kupitia vifaa vilivyochafuliwa kama nguo, shuka na vifaa vya hospitali. WHO imefafanua kuwa Ebola haisambazwi kupitia hewa kama Covid-19, lakini inaweza kuenea kwa haraka iwapo tahadhari hazitachukuliwa. Dalili za kwanza za Ebola ni pamoja na homa kali, uchovu, maumivu ya kichwa, koo na misuli. Baadaye mgonjwa anaweza kuanza kutapika, kuhara, maumivu ya tumbo na wakati mwingine kutokwa damu puani, mdomoni au sehemu nyingine za mwili. Kutokana na hali hiyo, Kenya imeongeza uchunguzi wa wasafiri wanaoingia nchini kutoka maeneo yaliyoathirika. Maafisa wa afya pia wamepewa mafunzo ya jinsi ya kutambua wagonjwa wanaoshukiwa kuwa na Ebola na namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi. WHO imeonya kuwa wafanyakazi wa afya wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ikiwa hatua kali za kujikinga hazitafuatwa. Tayari wahudumu kadhaa wa afya wamepoteza maisha katika mlipuko wa sasa. Hata hivyo, WHO inasema huduma za haraka hospitalini kama kuongeza maji mwilini, kudhibiti homa, kutibu maambukizi mengine na lishe bora huongeza nafasi ya wagonjwa kupona. Wataalamu pia wameonya kuwa baadhi ya watu wanaopona wanaweza kuendelea kuwa na virusi mwilini kwa muda mrefu, hasa kwenye shahawa, maziwa ya mama na baadhi ya viungo vya mwili. WHO imesisitiza kuwa kudhibiti Wizara ya Afya pia imewahimiza Wakenya kupata taarifa sahihi kuhusu Ebola kwa kupiga *719# au kupiga simu 719.
Original story
Continue reading at Taifa Leo (Swahili)
taifaleo.nation.co.ke
Summary generated from the RSS feed of Taifa Leo (Swahili). All article rights belong to the original publisher. Click through to read the full piece on taifaleo.nation.co.ke.
