Kenya
2,920 stories
Boost marine protection
Rising ocean temperatures, sea-level rise, and coastal storms continuously threaten shorelines,...
17 Jun 2026
Probe MP’s bias claim in port jobs recruitment
Using public jobs for political patronage is unlawful.
17 Jun 2026

President Ruto invites Arsenal after Kenyan fans celebrate title win
The North London side ended their 22-year wait for the Premier League crown at the end of May.
17 Jun 2026

Kuppet warns politicians as 61 teachers seek transfers over political tension
Ol Kalou campaigns stir fear among non-local teachers.
17 Jun 2026

Diana Wanza's dream for Commonwealth Games glory after Africa title gold
Kenya has not won the women’s 10,000 metres gold medal since Joyce Chepkirui’s success in 2014.
17 Jun 2026

At G7, Kenya reaches seafarers certification deal with Korea
The deal allows seafarers to require no additional certification to operate on ships reaching...
17 Jun 2026

North Rift: The guns are silent, but where is justice?
Ex-bandits are reintegrating into communities under the amnesty initiative, but a new dilemma...
17 Jun 2026

How NPS plans to dismantle political gangs
The new approach seeks to stop gang activities before they occur.
17 Jun 2026

Ocean Conference: 14 countries sign 'Mombasa Declaration' to fight illegal fishing
It advances transparency measures from the Global Charter to improve access and strengthen...
17 Jun 2026

G7 leaders pledge fresh funding to contain Ebola outbreak, says World Cup not at risk
They said the outbreak required urgent international attention.
17 Jun 2026

Court backs IEBC in diaspora voting rights battle
Court rejects a challenge by diaspora voters demanding expanded inclusion in the electoral...
17 Jun 2026

KOMBE LA DUNIA: Senegal kazi ngumu, naye Messi asisimua dunia
WAHAMIAJI na mashabiki wa kimataifa walisimama na Senegal kwenye kichapo cha 3-1 mikononi mwa Ufaransa kwenye mechi yao ya ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026 mnamo Jumanne usiku. Hii ni baada ya mashabiki wa Senegal kunyimwa viza za kuingia Amerika. Kocha Pape Thiaw alikuwa amesema kuwa alitarajia mashabiki wa Senegal wanaoishi jijini New York wangejitokeza kuwashabikia na kwa kweli walifanya hivyo. “Napiga kelele na natumai kuwa wachezaji wanaweza kunisikiza uwanjani. Kama nchi mwenyeji, inasikitisha sana kuona jinsi serikali yetu inawadhalilisha raia wa mataifa mengine,” akasema Shabiki Jessica Ambres, raia wa Amerika ambaye alivalia jezi ya Senegal. Amerika imezima mashabiki wa mataifa 39 yanayoshiriki kombe la dunia kuingia humo ikiwemo Iran, Haiti, Cote d’Ivoire na Senegal. Kuna idadi ya juu ya raia wa Haiti na Iran Amerika ile wale wa Senegal na Cote dIvoire ni wachache. Baada ya kipindi cha kwanza bila magoli, Ufaransa ilirejea kipindi cha pili kwa mori na kuyapata mabao yake kupitia Kylian Mbappe alifunga mabao mawili huku nguvu mpya Bradly Barcola ambaye aliingia nafasi ya Ousmane Dembele akifunga bao jingine. Senegal walipata bao lao kupitia fataki ya nguvu mpya Ibrahim Mbaye, 18. Matokeo hayo yana maana kuwa Senegal lazima ishinde mechi zake mbili zilizosalia ili kuwa na nafasi ya kutinga raundi ya 32. Lionel Messi naye alifunga mabao matatu mabingwa watetezi Argentina walipowakalifisha Algeria 3-0 katika Kundi J mnamo Jumatano asubuhi. Messi, 38, sasa ni mchezaji mkongwe zaidi kufunga kwenye Kombe la Dunia na bao hilo limekuja miaka 20 baada ya kuchezea Argentina kwa mara ya kwanza katika mashindano ya 2006. “Hii haielezeki na hakuna maneno ya kuyaeleza. Najua kuwa iwapo kuna mtu alifikiria kuwa timu hii ni bora kuliko Leo basi alinoa kwa sababu umuhimu wake ni dhahiri kwetu,” akasema Mac Allister. Argentina itacheza dhidi ya Austria mnamo Jumatatu kule Arlington, Texas nao Algeria wavaane na Jordan siku hiyo Santa Clara, California. Katika mechi nyingine, Austria ilipiga Jordan 3-1 kupitia mabao ya Marko Arnautovic, Romano Schimid na bao la kujifunga la Yazan Al Arab. Jordan walipata bao lao kupitia Ali Olwan.
17 Jun 2026

Africa’s anti-corruption research centre launched in Nairobi
The centre is both a vote of confidence in the country as 43 states back new graft war front.
17 Jun 2026

Aliyekuwa mhudumu wa benki anavyoigeuza nazi za Pwani kuwa ajira na utajiri
KATIKA ukanda wa Pwani unaojumuisha Kaunti za Kilifi, Kwale, Mombasa, Lamu, Tana River na Taita-Taveta, nazi zimeendelea kuwa zaidi ya zao la kitamaduni. Ni chakula, chanzo cha mapato na sehemu ya utambulisho wa jamii za pwani. Hata hivyo, biashara moja inayoongozwa na mwanamke imeanza kubadili mtazamo huo, ikithibitisha kuwa nazi zinaweza kuwa injini ya ajira na fursa mpya za kiuchumi, hasa kwa wanawake katika Uchumi Samawati unaokua nchini Kenya. Kupitia kampuni ya Nala Foods Africa Limited, mwanzilishi wake Subira Zingizi anachakata nazi kuwa bidhaa zenye thamani zaidi kama mafuta ya kupikia na ya vipodozi, pamoja na biskuti za nazi, hatua inayosaidia kuongeza mapato na kuimarisha ushiriki wa wanawake kwenye mtandao wa uongezaji thamani katika kilimo. Akiwa na umri wa miaka 37, Subira anasema safari yake ya ujasiriamali ilianza baada ya kufanya kazi katika sekta ya benki kwa zaidi ya miaka 10. Akiwa Shahada ya Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Kenyatta (KU), aliamua kuacha kazi ya ofisi na kuingilia biashara ya kuchakata mazao ya kilimo. Kwa sasa, akiwa na mwanzilishi mwenza na mkurugenzi mwenza Ali Salim Mbongi, wanaendesha kampuni inayojituma kuboresha kilimo cha nazi Pwani. “Tuliona pengo kubwa sokoni. Ingawa nazi hulimwa kwa wingi Pwani, bidhaa nyingi zinazouzwa madukani hazitoki Mombasa au Kwale,” Subira anasema. [caption id="attachment_189275" align="aligncenter" width="300"] Nazi zilizokunwa kwenye katika kampuni ya Nala Foods Africa. Picha|Sammy Waweru [/caption] Alianza biashara hiyo mwaka 2019 kwa mtindo usio rasmi, akinunua mafuta ya nazi kutoka kwa wanawake wa vijijini, kuyapakia upya na kuyauza kwa wateja. Wanawake hao, anasema, walikuwa na ujuzi wa jadi kuchakata nazi lakini walikosa masoko yenye ushindani mkuu na teknolojia ya kisasa ya uzalishaji. Mwaka 2022, biashara hiyo ilisajiliwa rasmi baada ya kupata ufadhili wa Sh50,000 kupitia mpango wa Youth Empowerment Product Initiative, fedha zilizotumika kusajili kampuni na kuingiza bidhaa sokoni. Katika hatua za mwanzo, uzalishaji ulikuwa wa mikono kabisa. “Wafanyakazi walikuwa wakikuna nazi kwa mikono, kuzikausha kwa kutegemea jua na kukamua mafuta bila mashine,” anasema, akieleza jinsi uzalishaji ulivyokuwa mgumu, wa gharama ya juu na wa polepole. Mabadiliko makubwa yalijiri baada ya kampuni hiyo kunufaika na mpango wa Investing in Women in the Blue Economy – Kenya, unaotekelezwa na Africa Enterprise Challenge Fund (AECF) kwa ushirikiano na Global Affairs Canada. Kupitia mpango huo, Nala Foods ilinunua mashine za kukama mafuta, kikaushio cha nishati ya jua na vifaa vingine vya kisasa vya uzalishaji. Subira anasema msaada huo uliibadilisha kampuni kutoka uzalishaji wa mikono hadi mfumo wa nusu-otomatiki. “Awali tulizalisha kati ya lita 20 na 50 kwa mwezi, lakini sasa tunazalisha angalau lita 200 kila mwezi,” anasema. Aidha, kampuni hiyo kwa sasa inaajiri wanawake kati ya 12 na 15 katika nyakati za uzalishaji, wakihusika na kukuna nazi, kukausha, kuchakata na kupakia bidhaa. Hali kadhalika, hununua nazi kutoka kwa wakulima na wasambazaji kutoka Kwale na maeneo jirani, hivyo kuimarisha uchumi wa ndani kwa ndani. [caption id="attachment_189276" align="aligncenter" width="300"] Vipodozi vilivyoundwa na Subira Zingizi kupitia Nala Foods Africa Limited. Picha|Sammy Waweru [/caption] Mbali na mafuta ya nazi, Nala Foods Africa Limited pia hutengeneza bidhaa za kujipodoa na biskuti za nazi, huku ikipanga kupanua zaidi uzalishaji wa vyakula na vitafunwa vinavyotokana na nazi. Kampuni hiyo pia imeanza kupenya masoko ya nje, Tanzania ikiwa mojawapo ya wanunuzi wake wakuu. Kwa sasa, takriban asilimia 20 ya uzalishaji wake huuzwa nje ya nchi. Subira anadokeza kwamba ongezeko la mahitaji linachochewa na mwenendo wa watu kukumbatia bidhaa asilia na lishe bora. Kulingana na mjasiriamali huyo, kuongeza thamani ya mazao ya shambani ndiyo njia muhimu kuhakikisha kilimo kinakuwa chanzo endelevu cha ajira na utajiri katika jamii za Pwani.
17 Jun 2026

PROF IRIBE: Ilifurahisha kumwona Rais Samia akitumia Kiswahili kuhutubu safu ya kimataifa
JUMA lililopita niliona kanda ya video ambapo Rais wa Tanzania Suluhu Samia Hassan alikuwa akizungumza Kiswahili katika safu ya kimataifa. Rais Samia alikuwa mshiriki katika mazungumzo ya jopo chini ya mwavuli wa Jukwaa la Kimataifa kuhusu maswala ya Kiuchumi la St Petersburg mnamo tarehe 5, Juni. Jopo hilo lilijumuisha Rais wa Urusi Vladimir Putin, Rais wa Uzbekistan Shavkat Mirziyoyev, Makamu wa Rais wa Uchina Han Zheng na Rais Samia. Mdhibiti wa jopo alikuwa mwanahabari anayetajika Geeta Mohan kutoka India. Mohan alimuuliza Rais Samia namna ambavyo angekwepa vikwazo ilivyowekewa Tanzania kaika azma yake ya kuongeza viwango vya biashara baina ya Tanzania na Urusi. Rais Samia alimjibu kwamba taifa la Tanzania halikuwa limewekewa vikwazo vya aina yoyote na yeyote. Bila shaka jibu hili lilimtia aibu huyo mdhibiti na kuashiria hali ya kutokuwa tayari au uchukulizi tu wa mambo bila kuyachunguza kwa kina. Lakini hilo silo lililonivutia katika mjadala huo. Lililonivutia ni yale maneno aliyoyasema Rais Suluhu kabla ya kutoa jibu hilo. Mdhibiti aliuliza swali lake kwa Kiingereza lakini kabla ya kulijibu, Rais Samia alimtaarifu kwa lugha iyo hiyo kwamba alivutiwa sana kuwasikia wanajopo wenzake wakichangia kwa kutumia lugha za taifa za nchi zao na kwa sababu hiyo, yeye pia angetumia nafasi yake kuzungumza kwa lugha yake ya taifa. Baada ya kutoa tahadhari hiyo, Rais Samia alianza kutoa jibu lake kwa lugha ya Kiswahili. Jambo hili lilinichangamsha si haba! Nimependekeza jambo hili mara nyingi. Nimekuwa nikisisitiza kwamba viongozi wetu watumie Kiswahili katika makongamano na mikutano ya kimataifa na katika kufanya hivi watawapa nafasi wakalimani kufanya kazi yao. Takriban mwaka mmoja uliopita niliandika hivi: “Ningetamani sana kuona hali kama hii Afrika: Rais Ruto akizungumza Kiswahili huku Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sis akitumia Kiarabu naye Nuhu Bakari akiwa mkalimani wao.” Niliendelea kuandika kwamba, inasikitisha sana kuwaona viongozi wetu wakitumia Kiingereza huku Mfaransa akitumia Kifaransa chake hivi kwamba mkalimani anayetumiwa ni wa Kiingereza-Kifaransa-Kiingereza. Mbona asiwe wa Kiswahili-Kifaransa-Kiswahili ilhali Kiswahili ni lugha rasmi nchini? Hii ndiyo sababu inayofanya nione raha kwamba pale palipotumiwa Kichina, Kirusi, Kiuzbeki na Kiingereza, Kiswahili pia kilipata nafasi yake kutokana na ukakamavu wa Rais Samia. Mwelekeo kama huu ukichukuliwa na viongozi wengine wa Afrika Mashariki, mbali na kuongeza ajira, uzalendo wa lugha pia utaimarika. Uzalendo wa lugha huenda sako kwa bako na uzalendo wa kiutamaduni na kijamii. Mwisho mwisho wa mwaka jana nilipendekeza pia kwamba wanaotuwakilisha katika ulingo wa kimataifa katika jambo lolote lile watumie Kiswahili katika majibu yao pasi kujali kama swali limeulizwa kwa lugha gani. Hivi, nilieleza, ndivyo tutakavyoheshimiwa na kudhihirishia ulimwengu kuwa tunaweza kuwasiliana kwa ufasaha bila kutapatapa au kuboronga sarufi na kanuni zingine za lugha. Hivi ndivyo alivyofanya Rais Samia. Kama wawakilishi wetu wakifanya mazoea ya kutumia Kiswahili, nilisema, basi vyombo vya habari ama vitatumia wakalimani au watafsiri kupata taarifa kwa lugha vinavyoipendelea. Katika kufanya hivi, wawakilishi hao watakuwa wamechangia pakubwa katika kueneza Kiswahili na kuunda nafasi za ajira kwa wanajumuiya wenzao.
17 Jun 2026

Africa's ocean moment cannot end in empty promises
Protecting the ocean is essential to feeding people, sustaining livelihoods, and securing a...
17 Jun 2026

The 20-year curse: Will a birthday goal end the World Cup drought this year?
There are 150 players at the 2026 Fifa World Cup whose birthdays fall during the tournament.
17 Jun 2026

Mswada wa kumpa Tshisekedi ‘Three Tam’ wapitishwa
KINSHASA, DR Congo: SENETI ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jana ilipitisha mswada wa kubadili katiba ambao una uwezo wa kumruhusu Rais Félix Tshisekedi kuhudumu kwa muhula wa tatu madarakani. Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya maandamano ya kupinga mswada huo kugeuka vurugu katika jiji kuu la Kinshasa.Mswada huo unafungua njia ya kufanyika kwa kura ya maoni kuhusu katiba mpya. Tshisekedi anahudumu muhula wake wa pili na wa mwisho kwa mujibu wa katiba ya sasa kugombea na kuhudumu muhula wa tatu. Maseneta 89 walishiriki katika kura hiyo iliyofanyika Jumatatu na wote walipiga kura kuunga mkono kupitishwa kwa mswada huo. Maseneta 20 hawakushiriki katika upigaji kura. Hata hivyo, mswada huo bado unahitaji kutiwa saini kuwa sheria na Rais Tshisekedi. Seneta wa upinzani, Salomon Kalonda Della Idi, alisema katika taarifa kwamba mswada huo unaweza kusambaratisha nchi. Wiki iliyopita, maandamano dhidi ya mswada huo yaligeuka vurugu wakati vikosi vya usalama vilipotumia vitoza machozi na kufyatua risasi hewani kuwatawanya waandamanaji. Waliokuwa wakishiriki maandamano walirusha mawe, Wandani wa mwanasiasa wa upinzani Delly Sesanga walidai kupitia mtandao wa X kwamba alipigwa risasi mguuni wakati wa vurugu hizo. Bunge la Kitaifa la DR Congo, ambalo ni bunge la chini, tayari lilikuwa limeidhinisha mswada huo kabla ya kupitishwa na Seneti. Uchaguzi mkuu ujao wa urais DR Congo umepangwa kufanyika mnamo 2028.
17 Jun 2026

Why High Court wants to examine Shakahola crime scene
Court will visit the alleged terror cells in Malindi where victims were allegedly accommodated...
17 Jun 2026

Kenya’s junior golfers go hunting in Japan World Cup
The team will represent Africa alongside the South African junior golf champions at this global...
17 Jun 2026

Ol kalou Chessboard: Political battle neither Gachagua, Kindiki wants to own
Kindiki wants to emerge as Ruto’s top ally in Mt Kenya, while Gachagua seeks to reaffirm his...
17 Jun 2026

Why Opposition named Natembeya their Western Kenya point man
The announcement was made by DCP leader Gachagua during a rally in Kitale on Sunday.
17 Jun 2026

Battle for Laikipia: Kiunjuri, Ndiritu, Waruguru in tight 2027 governor contest
Nine aspirants have declared interest in succeeding incumbent Governor Joshua Irungu.
17 Jun 2026

Lionel Messi's inexplicable feats no longer a surprise, says coach Scaloni
Messi's hat-trick at Kansas City Stadium saw him equal the all-time men's World Cup scoring...
17 Jun 2026

Retired England great Shearer tips African teams to do well in World Cup
The former striker is one of 18 football pundits that the BBC has hired for its World Cup...
17 Jun 2026

Covid-19 victim finally buried after six-year wait
The body was released to the family following a court order issued in Nakuru prohibiting the...
17 Jun 2026

Kenyans plan to ditch house helps buy machines as State pushes salaries to Sh18,000
Middle-class parents choose between hiring help and buying automated appliances.
17 Jun 2026

Meet the Migori nurse honoured by Ruto for transforming GBV survivor care
Working with survivors has transformed her life, exposing her to the realities of gender violence.
17 Jun 2026

Farmers turn to solar power to combat rising energy costs
Access to reliable and affordable power can mean the difference between making a profit and...
17 Jun 2026

Mke amegeuka DCI, anapekua simu na mifuko yangu kila nikiwasili nyumbani; nishauri
KILA ninaporudi nyumbani mke wangu hupenda kuangalia mfuko wangu, risiti nilizobeba na hata simu yangu. Anasema anafanya hivyo kwa sababu siku hizi watu wengi si waaminifu. Tatizo ni kuwa sijawahi kumpa sababu ya kunishuku. Sasa nahisi kama ninaishi na DCI. Nifanyeje bila kufanya mambo kuwa mabaya zaidi? Uaminifu ni msingi wa ndoa. Ikiwa mwenzako anaishi kama mpelelezi na mwingine kama mshukiwa, amani hupotea polepole. Zungumza naye kwa utulivu kuhusu jinsi unavyochukizwa na hiyo tabia yake. Jaribu kuelewa pia chanzo cha hofu yake. Wakati mwingine mashaka hutokana na majeraha ya zamani au ukosefu wa usalama wa kihisia. Mke ana tatizo la harufu kali na sijui nimuelezeje, naomba ushauri wako KUNA jambo ambalo sijawahi kumwambia mtu yeyote. Mke wangu amekuwa na tatizo la harufu ya mwili kwa muda sasa. Najua anaoga na kujitunza, lakini wakati mwingine harufu huwa kali sana. Naogopa kulizungumzia kwa sababu sitaki kumuumiza hisia. Lakini kimya changu pia kinaathiri ukaribu wetu. Nifanyeje? Mada kama hizi zinahitaji upendo, busara na heshima. Chagua muda mzuri wa kuzungumza naye faraghani na kwa lugha ya kujali. Usitumie maneno ya kumdhalilisha au kumlaumu. Wakati mwingine harufu ya mwili inaweza kuhusiana na afya, homoni au aina ya bidhaa zinazotumiwa. Mkaribie kama mke na rafiki anayejali ustawi wake, si mkosoaji. Mazungumzo ya heshima yanaweza kuleta suluhisho bila kuumiza uhusiano. Mwanangu ni mtundu ajabu, imekuwa kesi baada ya kesi, sijui nitamdhibiti vipi Shangazi, nina tatizo. Kila mara nina kesi kwa sababu ya mwanangu. Ana miaka 10 na amekuwa mkali sana na hupenda kupiga wenzake shuleni. Walimu wananilalamikia kila wiki. Sijui shida ni gani au kuna kitu kinamsumbua. Akienda shule, huwa najawa wasiwasi sana kwani kila simu kutoka shuleni ni malalamishi tu. Nimechoka sana. Nifanyeje? Tabia ya ukali kwa watoto mara nyingi ni ishara ya kitu kilichofichika, labda ni huzuni, hasira au mazingira. Zungumza naye kwa upole na muulize kinachomsumbua au kumtatiza moyoni. Pia chunguza mazingira yake ya nyumbani na shuleni. Adhabu pekee haitoshi; anahitaji kuelekezwa namna ya kueleza hisia zake bila vurugu. Kumbuka kuwa usipoziba ukuta sahii, utajenga ukuta baadaye maishani. Nakerwa na mume asiyependa kuoga Nimeolewa kwa miaka sita na kuna jambo linalonitesa kimya kimya. Mume wangu ni mtu mzuri, anajali familia. Tatizo ni usafi wake binafsi. Mara nyingi hurudi kutoka kazini akinuka jasho lakini hataki kuoga. Wakati mwingine huenda kulala bila kuoga kabisa. Hali hii imeanza kuniathiri hasa katika ukaribu wa ndoa yetu kwa sababu sipati hamu ya kuwa karibu naye. Nikijaribu kumwambia, huona kama namdharau au kumkosoa. Nifanyeje bila kumuumiza hisia zake? Usafi was kibinafsi si suala la anasa bali ni sehemu muhimu ya afya na mahusiano. Badala ya kumkosoa moja kwa moja, zungumza naye wakati mko katika hali nzuri na si wakati tatizo limetokea. Mweleze kuwa suala hili linakuathiri kihisia na hata ukaribu wa ndoa yenu. Tumia lugha ya upendo badala ya lawama. Wakati mwingine watu hawatambui jinsi tabia zao zinavyoathiri wenzao.
17 Jun 2026

Who is liable when surrogate baby is born with deformity?
Fertility clinics may face scrutiny where donor screening obligations were not adequately...
17 Jun 2026

Finance Bill 2026: Go to court or wait for Parliament? – Julius Rutto
17 Jun 2026
Teachers in Rachuonyo call for immediate govt intervention as school latrines near collapse
17 Jun 2026

Seneta lawamani kwa kusahau ‘waliomsaidia’
BAADHI ya wajumbe wa Chama cha ODM akiwemo Katibu wa ODM Voi, Bw Hassan Mwaniki, wamemlaumu Seneta Jonnes Mwaruma wakidai amewatenga licha ya kumsaidia uchaguzini, akilenga kuwania ugavana 2027. Hayo yalijiri huku wafuasi wa Chama cha ODM katika kaunti hiyo wakianza juhudi za kukipigia debe baada ya kupoteza viti vyote isipokuwa useneta na madiwani watano katika uchaguzi uliopita. Hata hivyo, Bw Mwaruma, aliwataka viongozi wa ODM kushirikiana na kuacha migogoro. Aliwahakikishia wajumbe kwamba chama kitaunda kamati ya uwiano ili kuwapatanisha mahasimu, na kujenga mshikamano ndani ya chama.
17 Jun 2026

Ruto pitches Africa ‘in a positive light’ as G7 leaders back debt reforms
Kenya’s President William Ruto revisited his familiar call for world leaders to see Africa as a...
17 Jun 2026

Purukushani kanisani ‘genge’ la vijana lilipovamia waumini eti kupima uthabiti wa imani yao
TUDOR, Mombasa VIJANA wa kanisa moja mtaani hapa walimwacha pasta wao akichana mbuga huku anapiga nduru, walipopanga kisanga cha kujaribu imani yake. Kila Jumapili pasta amekuwa akihimiza waumini wasiache imani hata wakikabiliwa na vitisho au mateso. Mahubiri yalipokuwa yakiendelea ghafla vijana 10 waliovaa vitambaa usoni waliingia kanisani na kutangaza wao ni genge la wahalifu. Waumini waliingiwa na hofu wakamtazama pasta. Alipoona hatari ikiwakodolea macho pasta aliruka kutoka jukwaani na kutimua mbio hadi nje akipiga mayowe akiomba msaada. Baada ya muda mchache vijana hao walivua vitambaa na kuanza kucheka. “Msihofu, sisi ni vijana wa kanisa hili. Tulitaka tu kupima kama pasta anaishi kulingana na mahubiri yake,” walitangaza huku waumini wakibaki mdomo wazi wamepigwa na butwaa.
17 Jun 2026

Gusii glass ceiling: Woman reps Donya, Jerusha dare 60-year elective jinx
Both trailblazing candidates must navigate deeply rooted patriarchal traditions.
17 Jun 2026

Deputy principals turn to Parliament as TSC races to review career progression guidelines
The TSC has until the end of June to finalize and publish an updated career guideline.
17 Jun 2026

How a tech startup is turning 9 years of HR frustration into Kenya’s secret competitive weapon
They have chosen Nairobi as its regional hub to deploy agentic AI tools across East Africa...
17 Jun 2026

Kenya wants to close refugee camps: the promise and risks
Now, the country is attempting a major shift in refugee policy.
17 Jun 2026

Cofek yakimbia kortini kuzima vipengee tata kwenye Mswada wa Fedha 2026
SHIRIKISHO la Watumiaji bidhaa nchini (Cofek) limewasilisha kesi katika Mahakama Kuu likitaka kuondolewa kwa baadhi ya vipengele vya Mswada wa Fedha wa 2026, likidai vinaweza kuongeza gharama ya maisha na kuhatarisha haki za walipa ushuru. Katika kesi iliyowasilishwa katika Kitengo cha Katiba na Haki za Kibinadamu, Cofek inataka mahakama izuie utekelezaji wa vipengele hivyo iwapo Bunge litavipitisha kuwa sheria. Shirikisho hilo linaonya kuwa kuondolewa kwa msamaha wa Ushuru wa Ongezeko la Thamani (VAT) kwa baadhi ya bidhaa muhimu kutasababisha kupanda kwa bei za vyakula, bidhaa za afya, pembejeo za kilimo na vifaa vya elimu, huku mzigo huo ukibebwa na watumiaji bidhaa. Aidha, Cofek inaeleza kuwa mapendekezo ya kupanua nguvu za Mamlaka ya Ushuru Kenya (KRA) inaweza kuruhusu utozaji wa ushuru bila taratibu za haki, ikiwemo kuondoa nafasi ya kusikilizwa.
17 Jun 2026

Maraga: Kuondoa Ruto hakutoshi, lazima tung’oe mizizi inayoleta mafidhuli uongozini
MGOMBEA urais wa chama cha United Green Movement (UGM), David Maraga, ametoa wito kwa vyama vya upinzani kuungana kwa misingi ya maadili, utawala wa sheria na kuheshimu Katiba, akisema Kenya inahitaji mwanzo mpya ili kukabili ufisadi, kudorora kwa uchumi na kuporomoka kwa taasisi za umma. Akizungumza katika hotuba yake ya Hali ya Taifa aliyotoa akiwa Ufungamano House, Nairobi, baada ya kukamilisha ziara aliyoita ‘Ukatiba Caravan’ katika kaunti 43, aliyekuwa Jaji Mkuu alisema uchaguzi mkuu wa 2027 utakuwa wa kuamua hatima ya nchi. “Ninaamini katika umoja wa upinzani, lakini umoja huo lazima ujengwe kwa misingi ya maadili na si tamaa ya madaraka. Lazima tuungane chini ya utawala wa sheria ili kuhakikisha hakuna kiongozi atakayetumia mamlaka vibaya kupora rasilimali za umma, kuua watoto wetu au kuzima sauti za wakosoaji,” alisema. Bw Maraga alisema safari yake ya kuzunguka nchi ilimfanya ashuhudie malalamishi mengi kutoka kwa wananchi kuhusu ufisadi uliokithiri, ukosefu wa ajira, gharama ya juu ya maisha na kuzorota kwa huduma za afya na elimu. Alisema Wakenya walionyesha kuwa bado wana matumaini licha ya changamoto wanazopitia, lakini walilalamikia kupuuzwa kwa utawala wa sheria, kuingiliwa kwa taasisi za umma na kuendelea kwa ufisadi. Kwa mujibu wake, viongozi wameisaliti ndoto ya waanzilishi wa taifa kwa kugeuza serikali kuwa njia ya kujinufaisha wao wenyewe, familia zao na washirika wao. Bw Maraga alimshutumu Rais William Ruto kwa kile alichodai kuwa kuendeleza ufisadi na kuongeza deni la taifa kupita kiasi, akisema karibu nusu ya bajeti ya serikali sasa inaelekezwa kulipa madeni. Katika mpango wake wa kuongoza Kenya, Bw Maraga alisema serikali yake itajikita katika nguzo tatu za kurekebisha, kurejesha na kujenga upya taifa. Aliahidi kuimarisha taasisi za umma, kuheshimu Katiba, kukomesha mauaji ya kiholela na kukabiliana vikali na ufisadi. “Nitahakikisha Katiba ndiyo mwongozo mkuu wa serikali yangu. Hakutakuwa na aliye juu ya sheria,” alisema. Aidha aliahidi kufufua uchumi kupitia kilimo, viwanda na ubunifu wa teknolojia huku akiwapa vijana nafasi zaidi za ajira na matumizi ya Akili Unde (AI). Maraga alisema hajawahi kuhusishwa na kashfa yoyote ya ufisadi na yuko tayari kutangaza mali yake hadharani, akiwataka wagombeaji wengine wa urais kufanya vivyo hivyo. “Kuondoa Rais Ruto pekee hakutoshi. Lazima tubadili mfumo mzima wa uongozi. Serikali ijayo isiwe mchezo wa kubadilishana viti huku watu walewale wakiendelea kujinufaisha,” alisema. Katika mkutano huo, viongozi mbalimbali wa upinzani akiwemo Martha Karua, Caleb Amisi, Wilberforce Oundo na Caroli Omondi walisisitiza umuhimu wa kuungana ili kuondoa nchi katika matatizo ya sasa na kujenga uongozi unaozingatia uwajibikaji na maslahi ya wananchi.
17 Jun 2026

Nassir aagiza mpango wa lishe shuleni ukaguliwe baada ya malalamishi kushamiri
GAVANA wa Mombasa, Bw Abdulswamad Nassir, ameagiza ukaguzi wa mpango wake wa lishe kwa wanafunzi wa shule za sekondari za kutwa, uliolenga kupunguza gharama ya karo ya shule kwa wazazi. Hii ni baada ya wazazi kulalamika kwamba bado wanalipa karo ya juu licha ya mpango huo wa serikali ya kaunti, huku mamia ya wanafunzi wakiendelea kufukuzwa shule kwa kutolipa karo. Bw Nassir ameagiza maafisa wa kaunti kuanza ukaguzi wa mpango huo ili kubaini ukweli. Maafisa hao watawahoji wazazi, wanafunzi, walimu na wasimamizi wa shule hizo ili kutathmini utekelezaji wa mpango huo. Zoezi hilo, linalotarajiwa kuanza wiki hii, linalenga kubaini iwapo mpango huo unafanikisha malengo ya kuboresha sekta hiyo na kupunguza gharama za masomo ya sekondari. Bw Nassir alisema anataka kupata maoni ya moja kwa moja kutoka kwa walengwa. Chini ya mpango huo, wanafunzi wa shule za sekondari za kutwa hupatiwa chakula kinachofadhiliwa na serikali ya kaunti, huku gharama ya ada ikitarajiwa kushuka kutoka Sh22,000 hadi Sh12,000 kwa mwaka. “Tulipoanzisha mpango huu, lengo lilikuwa kuboresha elimu na kuhakikisha watoto wanapata lishe bora na kupunguza mzigo wa kifedha kwa familia kwa takriban Sh12,000 kwa kila mwanafunzi kwa mwaka. Sasa tunataka kubaini hali halisi,” alisema. Alitoa wito kwa wazazi, wanafunzi na wadau wa elimu kushirikiana na serikali yake ya kaunti kutoa maoni ya kweli kuhusu mafanikio na changamoto za mpango huo.
17 Jun 2026

G7 endorses joint France-UK naval mission to clear Iranian war mines
The G7, born of the oil shock of 1973 to help manage economic crises, is now ducking the...
17 Jun 2026

Magenge ya wahuni sasa yawinda wanasiasa na viongozi katika mikutano ya kisiasa
MIKUTANO ya kisiasa nchini inazidi kuwa uwanja wa mawindo kwa magenge ya wahalifu wa kulipwa, huku wanasiasa, viongozi wa hadhi ya juu na timu zao za kampeni wakilengwa kwa wizi na uporaji. Mashirika ya usalama yameonya kuwa magenge ambayo hapo awali yalijulikana kwa kufuata misafara ya viongozi wa kisiasa na kudai pesa za kampeni sasa yamebadilika na kuwa mitandao ya uhalifu iliyojipanga vyema. Makundi hayo hutumia vurugu na msisimko wa mikutano ya kisiasa kuwaibia viongozi na wasaidizi wao fedha, simu za mkononi, vito na mali nyingine za thamani. Maafisa wa usalama wanasema hali hiyo inatia wasiwasi mkubwa. Katika eneo la North Rift, hasa. Kaunti ya Uasin Gishu, tatizo hilo limeongezeka kiasi kwamba mamlaka sasa zinachukulia kama tishio kubwa kwa usalama huku shughuli za kisiasa zikitarajiwa kushika kasi kutokana na miungano na mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea. “Tunakumbwa na changamoto ya ongezeko la wahuni wanaoning’inia magari ya viongozi wakuu wakidai motisha zisizo halali,” alionya Kamishna wa Kaunti ya Uasin Gishu, Dkt Eddyson Nyale. Hata hivyo, maafisa wa usalama wanasema tatizo hilo si la vijana wanaotafuta pesa pekee. Uchunguzi unaonyesha kuwa baadhi ya magenge huingia katika mikutano ya kisiasa yakijifanya wafuasi au walinzi binafsi wa viongozi maarufu. Wakiwa ndani ya umati, hutumia msongamano unaotokana na kuwasili kwa viongozi kutekeleza wizi. Akizungumza katika mkutano wa umma eneo la Tarakwa, Kaunti Ndogo ya Kesses, Dkt Nyale alisema utawala wa eneo hilo hautavumilia tena ongezeko la vitendo vya kihuni. “Hatutakaa na kukunja mikono huku wazururaji na wahuni wakiendelea kujihusisha na shughuli za uhalifu,” alisema. Aliongeza kuwa kile kinachoonekana kama shamrashamra za kawaida za kuwakaribisha viongozi sasa kimekuwa maficho ya wahalifu. “Kuning’inia magari yanayoendeshwa si kosa la trafiki na hatari kwa usalama pekee, bali pia kumekuwa njia ya kutekeleza uporaji na unyang’anyi. Tumeagiza polisi kuwakamata wote watakaopatikana wakizunguka au kuning’inia kwenye misafara ya viongozi wa kisiasa,” alisema. Kwa mujibu wa Kamishna huyo, taarifa za kijasusi zinaonyesha baadhi ya vijana hao huandaliwa na wanasiasa hasimu kuvuruga mikutano au kuonyesha kana kwamba wanaungwa mkono kwa wingi. Hata hivyo, wengi wao sasa wamegeuza mikutano hiyo kuwa fursa ya kutekeleza wizi. Onyo hilo linajiri huku kukiwa na hofu kuhusu kurejea kwa siasa za kutumia wahuni katika maeneo mbalimbali nchini. Katika wiki za hivi karibuni, video kutoka mikutano ya kisiasa katika kaunti za Uasin Gishu, Trans Nzoia na Nandi zimeonyesha makundi ya vijana yakizingira kwa fujo magari ya viongozi, wakining’inia misafara inayosonga, wakifungua milango kwa nguvu na kusukumana karibu na viongozi wakidai wanawakaribisha. Baadhi ya viongozi tayari wameathirika. Mwezi Mei, Mbunge wa Mogotio Reuben Kiborek alifichua hadharani kuwa simu yake ya mkononi iliibwa alipohudhuria mazishi ya babake Waziri wa Barabara na Uchukuzi, Davis Chirchir katika Kaunti ya Bomet. Baadaye mbunge huyo aliandika kwenye mitandao ya kijamii akiwaomba walioiba simu hiyo wamrudishie. “Lakini watu wa Bomet, mbona mniibie simu na vile nyinyi ni watu wangu. Sharp boys,” aliandika huku akiwaita washukiwa hao “sharp boys” na hata kuahidi zawadi kwa atakayerudisha simu hiyo. Maafisa wa usalama wanaamini kuwa wizi huo ni sehemu tu ya mtandao mpana wa uhalifu unaokua sambamba na shughuli za kisiasa. Dkt Nyale alifichua kuwa baadhi ya magenge hayo pia yamepanua shughuli zao na sasa yanawalenga madereva wa magari ya kibiashara.
17 Jun 2026

Former Taita Taveta political director arrested by EACC
He will be arraigned today at Voi Anti-Corruption Court.
17 Jun 2026

Teen volleyball sensation Milka Akinyi calls the shots at Pipeline
High school student hungry for success with Kenya Pipeline women's volleyball team.
17 Jun 2026

Mkewe Uhuru, nduguze 3 wavutania mali na mjane wa kaka yao mdogo
ALIYEKUWA Mama wa Taifa Margaret Kenyatta amejitosa katika mzozo wa kisheria kuhusu urithi wa mali ya ndugu yake marehemu, William Gakuo Njuguna, akishirikiana na ndugu zake watatu kupinga mjane wa marehemu kuhusu usimamizi wa mali hiyo. Bi Margaret Kenyatta pamoja na Peter Maina Gakuo, Gabriella Njeri Gakuo na Christine Wambui Gakuo, wanataka Mahakama Kuu kubatilisha hati ya usimamizi wa mali iliyotolewa kwa mjane wa marehemu, Sheila Wanjiku Mwangi, wakidai ilipatikana kwa njia ya udanganyifu na kwa kuficha taarifa muhimu. Wanadai kuwa mahakama haikufahamishwa kwamba wao ni baadhi ya ndugu wa karibu waliobaki wa marehemu na hivyo walinyimwa nafasi ya kushiriki katika mchakato wa urithi. Hata hivyo, wakili wa Bi Mwangi, Bw Erick Mutua, amepinga madai hayo akisema ndugu hao hawana haki ya kisheria ya kurithi mali hiyo chini ya Sheria ya Urithi. Bw William Gakuo Njuguna, mdogo wa Bi Kenyatta, alifariki mnamo Novemba 2024 nyumbani kwake Karen, Nairobi akiwa na umri wa miaka 48. Stakabadhi za mahakama zinaonyesha kuwa alikufa bila kuacha watoto. Mali yake inajumuisha ardhi Kaunti ya Narok, hisa katika kampuni za Siaya Greens Limited, Tinderet Greens Limited na Kenindia Assurance Company Limited, gari aina ya Mitsubishi Pajero pamoja na mgao kutoka kwa mali ya marehemu babake, Ephantus Gakuo. Mali hiyo inakadiriwa kuwa ya thamani ya Sh50 milioni. Bi Mwangi aliomba Mahakama Kuu apewe mamlaka ya kusimamia mali hiyo akijitambulisha kama mke wa marehemu na mrithi pekee aliyebaki. Hati hiyo ilitolewa Desemba 2025. Lakini Peter Maina Gakuo, kwa niaba ya ndugu zake, ameomba hati hiyo ifutiliwe mbali, akisema ilipatikana kwa kuficha ukweli kuhusu watu wengine waliokuwa hai na wenye maslahi katika urithi huo. “Barua ya usimamizi ilipatikana kwa njia ya udanganyifu kupitia kufichwa kwa makusudi kwa taarifa muhimu kuhusu watu waliobaki baada ya kifo cha marehemu,” walieleza katika maombi yao. Bi Mwangi amekanusha madai hayo, akisema walalamishi hawakuwa wakitegemea marehemu kwa mujibu wa Sheria ya Urithi na hivyo hakuhitajika kuwataja katika ombi lake. Katika hati yake ya kiapo ya kujibu kesi, alisema waombaji hao hawajathibitisha kuwa wana haki yoyote ya kisheria, walikuwa wakimtegemea marehemu au kulikuwa na udanganyifu katika mchakato huo. “Mbali na kukosoa namna ombi lilivyowasilishwa, hawajaonyesha kuwa wana haki yoyote ya kunufaika na mali ya marehemu,” alisema. Aidha alibainisha kuwa ndugu hao ni watu wazima wanaojitegemea kifedha, akitaja kuwa Margaret Kenyatta ni mke wa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta. Wakili Erick Mutua aliunga mkono msimamo wa mjane huyo, akisema ombi la kubatilisha hati hiyo halina msingi wa kisheria na limewasilishwa kwa nia mbaya ili kuendeleza maslahi katika mgogoro mwingine tofauti. Wakati huo huo, Bi Mwangi amedai kuwa amefungiwa nje ya nyumba yake ya ndoa iliyoko Karen na kunyimwa nafasi ya kuchukua nguo na mali zake binafsi. Pia anadai mfanyakazi wake wa bustani alifukuzwa kwa nguvu. Katika madai mengine mazito, alisema mumewe alijitoa uhai kutokana na msongo wa mawazo uliotokana na kutopata sehemu yake ya urithi wa mali ya babake, Ephantus Gakuo. “Alijihisi kutengwa na kuvunjika moyo kwa kuwa alikuwa mtoto pekee wa mama tofauti na waombaji, hali iliyomfanya kuamua kujiua Novemba 7, 2024,” alidai. Bi Mwangi pia amewashutumu wasimamizi wa mali ya marehemu Ephantus Gakuo kwa kushindwa kutoa maelezo kuhusu takriban Sh300 milioni zilizopatikana kutokana na mauzo ya ardhi katika eneo la Bamburi North kwa serikali, madai ambayo bado hayajathibitishwa mahakamani. Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 2, 2026.
17 Jun 2026

Ahero irrigation scheme set for Sh5.1bn upgrade
Established in 1966, the Ahero Irrigation Scheme is one of Kenya's oldest public irrigation...
17 Jun 2026

'How beef credit to my landlady turned into a costly lesson on rent and debt'
What started as an act of goodwill turned into a financial headache for Kisumu businessman.
17 Jun 2026

New Jersey Notebook: Ghana’s coach Quiroz matches World Cup record
Queiroz will be looking to guide Ghana past their quarter-final achievement of 2010.
17 Jun 2026

From sweetheart to official names: The stories hidden in our contact lists
An encounter about saved phone contacts uncovered deeper lessons about identity, respect...
17 Jun 2026

Stunned silence in court as video of Tob Cohen crime scene shown
Graphic details from the crime scene where Cohen's body was recovered laid bare in court.
17 Jun 2026

Finance Bill pressure turns House into theatre of shouting matches
Lawmakers clash in the House over the proposed tax measures in contentious Bill.
17 Jun 2026

Disquiet in ODM amid claims of sidelining in Sh2bn victims pay
Oburu Oginga complains in public that he was not properly invited to State House function.
17 Jun 2026

Students petition MPs for representation to curb schools unrest
Students forum seeks the establishment of structured learners consultation mechanisms.
17 Jun 2026

Thousands of varsity students to miss funding as Helb runs short
Government allocated only a fraction of the money required to university students' education.
17 Jun 2026

History-making DR Congo eye Portugal scalp
DR Congo up against Cristiano Ronaldo-led Portugal in their group opener.
17 Jun 2026

ODM machozi tu, yadai kupigwa kumbo na UDA katika fidia ya waathiriwa wa maandamano
MVUTANO wa wazi kati ya chama tawala cha UDA na ODM kuhusu fidia kwa waathiriwa wa maandamano ulijitokeza katika Ikulu Jumatatu iliyopita baada ya Seneta Oburu Oginga kulalamikia kile alichodai ni kutengwa kwa chama chake. Dkt Oginga, ambaye ni kinara wa ODM, alimwambia hadharani Rais William Ruto kuwa mwaliko wake kuhudhuria hafla ya kupokelewa kwa ripoti ya Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu (KNCHR) kuhusu mfumo wa kufidia waathiriwa wa ukiukaji wa haki za binadamu ulionekana kutolewa dakika za mwisho. Imebainika kuwa Dkt Oginga alipokea mwaliko wa kuhudhuria hafla hiyo Jumatatu asubuhi na alipowasili shughuli zilikuwa tayari zimeanza. Viongozi kutoka mihimili yote mitatu ya serikali – Serikali Kuu, Bunge na Mahakama – walikuwa wamehudhuria. Mbali na Dkt Oginga, Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa Junet Mohammed ndiye afisa mwingine pekee wa ODM aliyekuwa Ikulu. Baadhi ya maafisa wa ODM walidai Bw Mohammed alihudhuria kwa bahati tu baada ya kufika Ikulu kushuhudia kutiwa saini kwa Mswada wa Ugavi wa Mapato wa 2026, huku maafisa wa Ikulu wakisema alialikwa kama sehemu ya uongozi wa Bunge. Fidia kwa waathiriwa wa maandamano ilikuwa mojawapo ya ajenda 10 zilizotiwa saini kati ya Rais Ruto na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga Machi 7, 2025. Viongozi wa ODM wanaamini chama hicho kinapaswa kushirikishwa kikamilifu katika utekelezaji wa mpango huo kama ishara ya nia njema. Makubaliano ya kisiasa kati ya UDA na ODM yanategemea ajenda hiyo ya vipengele 10 inayolenga kuongoza mageuzi katika utawala, ushirikishaji wa kiuchumi, uaminifu uchaguzini na uwajibikaji wa taasisi za umma. ODM imekuwa ikitumia ahadi ya kufidia familia za waliouawa na waliojeruhiwa na polisi wakati wa maandamano ya kupinga serikali kuvutia wafuasi wake kuunga mkono serikali jumuishi na hata uwezekano wa kumuunga mkono Rais Ruto katika uchaguzi mkuu ujao. Alipopewa nafasi ya kuzungumza, Dkt Oginga hakusita kueleza kutoridhishwa kwake na jinsi ODM ilivyoshughulikiwa katika hafla hiyo. “Kwanza kabisa, Mheshimiwa Rais, ningependa kusema sikuandaliwa ipasavyo kwa hafla hii. Sijui kwa nini sikualikwa kwa wakati unaofaa, lakini sitaki kulalamika,” alisema. Aliendelea kusema kuwa huenda hali hiyo ilitokana na kutokuwapo kwa ndugu yake Raila Odinga. “Nadhani ni kwa sababu ndugu yangu hayupo. Angekuwepo nina hakika angekuwa wa kwanza kualikwa kwa sababu alithamini sana masuala ya haki za binadamu,” alisema. Baadaye Dkt Oginga alieleza kuwa mpango wa kufidia waathiriwa ni mradi uliokuwa karibu sana na moyo wa Bw Odinga. "Kwa ushirikiano na serikali nitahakikisha kila mtu anayestahili anafidiwa. Kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, tafadhalini pokeeni hili kama ishara ya majuto; ingawa maisha ya binadamu hayawezi kulipwa kwa fedha, ni hatua muhimu kuelekea haki,” alisema. Bw Mohammed alikataa kutoa maoni kuhusu suala hilo alipofikiwa na wanahabari wetu. Hata hivyo, afisa mmoja wa ODM alisema Bw Mohammed na mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge walifahamishwa kuhusu mkutano huo walipofika Ikulu kwa shughuli ya kutiwa saini kwa Mswada wa Ugavi wa Mapato. “Hakuna afisa wa chama aliyealikwa. Manaibu viongozi wa chama, Magavana Simba Arati wa Kisii na Abdulswamad Nassir wa Mombasa pamoja na mwenyekiti wa chama Gladys Wanga hawakupata mwaliko,” alisema afisa huyo. Jinsi hafla hiyo ilivyoandaliwa imezua mjadala mkali ndani ya ODM, huku baadhi ya viongozi wakidai kuwa kuna njama ya UDA na Rais Ruto kujijenga na mpango wa fidia. Suala hilo lilijadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ya Usimamizi ya ODM kilichofanyika Jumatatu jioni na kuhudhuriwa na Dkt Oginga, Magavana Arati, Wanga na Nassir, Bw Mohammed, Naibu Katibu Mkuu Catherine Omanyo, Gavana wa Wajir Ahmed Abdullahi na Mweka Hazina Timothy Bosire miongoni mwa wengine. “Fidia hii ilikuwa wazo la ODM na inamilikiwa kwa pamoja na vyama vyote viwili,” alisema mmoja wa waliohudhuria kikao hicho. Aliongeza kuwa kauli ya Rais Ruto kwamba rafiki yake alimuonya kuwa kufidia waathiriwa kungeonekana kama kukiri makosa ilionyesha juhudi za kuufanya mpango huo kama ni wa kibinafsi. “Hotuba ya Oburu ilikuwa ishara tosha kuwa chama hakijafurahishwa na jinsi suala hili linavyoshughulikiwa,” alisema. Kwa upande mwingine, afisa mmoja wa Ikulu aliyezungumza kwa sharti ya kutotajwa jina alisema mpango wa awali ulikuwa KNCHR iwasilishe ripoti yake kwa Rais katika kikao kidogo cha ofisini Ijumaa, lakini Rais akaagiza hafla ya hadhara kufanyika Jumatatu. Alisema mkanganyiko ulitokea baada ya mwaliko kutolewa kwa viongozi wa Bunge na Mahakama pekee, akifichua pia kuwa Rais mwenyewe alimpigia simu Dkt Oginga Jumatatu asubuhi kuuliza kama alikuwa amealikwa. “Lengo lilikuwa kikao kidogo cha kuwasilisha ripoti, lakini Rais alisema kwa kuwa suala hilo linahusu fedha za umma lifanywe hadharani,” alisema afisa huyo. Katika hotuba yake, Rais Ruto alisema mpango huo unatokana na imani ya pamoja kwamba Kenya haiwezi kuendelea kupitia maumivu yale yale kizazi baada ya kizazi na maandamano baada ya maandamano. Ripoti hiyo inahusu ukiukaji wa haki za binadamu uliotokana na maandamano miaka ya 2017, 2022, 2023, 2024 na 2025, yakiwemo maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha na yale ya vijana wa Gen Z pamoja na maandamano ya Saba Saba.
17 Jun 2026

Reparations for victims of protests; Ruto's political card or genuine concern?
17 Jun 2026
